Mkuu wa mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi akimuapisha Mkuu wa Wilaya ya Ikungi,Mh Edward Mpogolo leo Ofisini kwake,mara baada ya kuteuliwa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt John Pombe Magufuli .Mh Edward alikuwa Katibu Tawala Wilaya ya Dodoma. 
 Mkuu wa mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Ikungi,Mh Edward Mpogolo vitendea kazi leo Ofisini kwake,mara baada ya kuteuliwa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt John Pombe Magufuli.Mh Edward alikuwa Katibu Tawala Wilaya ya Dodoma. 
 Mkuu wa Wilaya ya Ikungi,Mh Edward Mpogolo akitia saini kiapo chake mara baada ya kuapishwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida Mh Dkt.Rehema Nchimbi.



Na Charles James, MICHUZI TV

MKUU mpya wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida, Bw Edward Mpogolo ameapishwa leo rasmi kuanza majukumu yake kama Mkuu wa Wilaya hiyo, kuchukua nafasi ya iliyoachwa wazi na Miraji Mtaturu ambaye kwa sasa ni Mbunge wa jimbo la Singida Mashariki.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ikulu jana, uteuzi wa Bwana Mpogolo ulianza rasmi jana Julai 24, 2019, kuwa mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida.

Baada ya kuapishwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Bi Rehema Nchimbi, Mpogolo ameahidi kushirikiana na uongozi wa Halmashauri ya  Wilaya katika  kuhakikisha inakuwa na maendeleo sambamba na kusimamia kikamilifu  makusanyo  ili kuinua uchumi wa eneo hilo.

“Ninamskuru Rais Dk,John Magufuli kwa kuniteua,ninaahidi kuwa sitamwangusha ,nitahakikisha ninashirikiana na Uongozi wa Mkoa na Halmashauri yangu ya Ikungi ili kuhakikisha tunafikia malengo ya makusanyo katia Wilaya yetu”amesema Mpogolo.

Ameahidi kushirikiana na uongozi wa halmashauri ya Wilaya ya Ikungi ili kuhakikisha wanatumikia wananchi wa Wilaya hiyo ikiwa wao ndio wawakilishi wa Rais katika eneo hilo.

Pia ameahidi kwenda kuisimamia  Katiba ya Nchi pamoja na Ilani ya Chama Tawala, Chama Cha Mapinduzi  katika  kuwatumikia   wananchi atakaowaongoza.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk. Rehema Nchimbi amesema  Mkuu wa Wilaya ndio msimamizi mkuu wa Kamati ya ulinzi na usalama na ndio msimamizi mkuu wa shughuli za maendeleo katika eneo husika na kumtaka kwenda kusimamia  vyema miradi ya Serikali inayotekelezwa Wilayani humo.

“Mkuu wa Wilaya yeye ni msimamizi mkuu na muwakilishi wa Rais katika Wilaya na ndio mkuu wa kamati ya ulinzi na usalama na ukasimamie miradi yote inayotekelezwa Wilayani humo” amesema Dtk Rehema.

Hata hivyo amemwambia kuwa Wilaya ya Ikungi inamiradi mbalimbali ya maendeleo iliyokusudiwa kwenye malengo ikiwemo miradi ya visima 28 vilivyokusudiwa kukamilishwa .

Aidha Dk.Nchimbi amesema upande wa Singida magharibi wana miradi ya visima 13 na Singida mashariki visima 15 .

Amebanisha malengo mengine yaliyowekwa kwa Wilaya hiyo kuwa ni kilimo cha zao la michikichi ekari 200 pamoja na kilimo cha zao la korosho.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...