Wafanyakazi hospitali ya Wilaya ya Meru, watendaji na wadau wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya Jerru Muro (hayupo pichani), wakati wa uzinduzi wa kampeni ya jiongeze tuwavushe salama katika ukumbi wa Halmashauri ya Meru.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro akisaini hati ya kiapo kati yake Mkuu wa Wilaya ya Maafisa Tarafa wa tarafa za Mbuguni, Poli na King’ori kuhakikisha kampeni ya kuzuia vifo vya Mama na Mtoto vinafanikiwa. Aliyesimama nyuma wa tatu kutoka kushoto ni Mganga Mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Meru, Dkt Maneno Focus.
Wafanyakazi hospitali ya Wilaya ya Meru, watendaji na wadau wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya Jerru Muro (hayupo pichani), wakati wa uzinduzi wa kampeni ya jiongeze tuwavushe salama katika ukumbi wa Halmashauri ya Meru.
Wafanyakazi hospitali ya Wilaya ya Meru, watendaji na wadau wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya Jerru Muro (hayupo pichani), wakati wa uzinduzi wa kampeni ya jiongeze tuwavushe salama katika ukumbi wa Halmashauri ya Meru.
Na Seif Mangwangi , Michuziblog, Arusha
SERIKALI wilayani Arumeru imefanikiwa kupunguza vifo vya Mama na Mtoto kufuatia kuboresha huduma za afya wilayani humo ikiwemo dawa na vifaa muhimu vinavyotumika wakati Mama anajifungua.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni maalum ya Kitaifa ya kuzuia vifo vya Mama na Mtoto inayojulikana kwa jina la ‘ Jiongeze, tuwavushe Salama’, iliyofanyika katika ofisi za Halmashauri ya Meru, Mganga Mkuu wa Halmashauri hiyo Wilayani Arumeru Dkt. Maneno Focus alisema huduma hizo zimeboreshwa kwa asilimia 98.
“Katika Wilaya yetu tunataka kutokomeza kabisa vifo vya Mama na Mtoto na tunafanya hivi kwa vitendo, katika kipindi cha Januari hadi Juni 2019 tumepata vifo viwili pekee vya Watoto ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka 2018 ambapo watoto 5 walikuwa wamefariki,”alisema
Amesema pamoja na takwimu hizo bado kumekuwa na changamoto ya upatikanaji wa taarifa sahihi na kwa wakati kutoka kwenye jamii hususani kwa wazazi ambao hawafiki kwenye vituo vya afya kwaajili ya kupata huduma.
Dkt Maneno alisema kampeni hiyo imelenga kuongeza uwajibikaji wa viongozi wa kisiasa, kidini, kijamii na wadau wote kuwajibika na kuhakikisha vifo vya Mama na Mtoto vinadhibitiwa na kufuatiliwa na kila mmoja kushiriki kuvizuia.
“Halmashauri ya Meru inatarajia kuongeza huduma jumuishi za Kujifungulia (CeMonc), katika kituo cha afya cha USA – RIVER, ambacho majengo ya huduma muhimu yamekamilika, tunaamini hadi kufikia mwakani hakutakuwa na vifo vya Mama wala Mtoto wilayani kwetu,”anasema.
Mgeni rasmi katika uzinduzi huo Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro anasema Wilaya ya Arumeru imeazimia kuboresha huduma za Afya na mikakati iliyopo ni kuhakikisha kila kata inakuwa na kituo cha afya na kila kijiji kinakuwa na zahanati.
Muro aliwaagiza viongozi wa Hospitali ya Meru kutoa matangazo ya katazo la watendaji wa afya hospitalini hapo kutumia simu wakati wa kazi na kuwataka kutumia lugha nyenyekevu kwa wagonjwa na kwamba kwa kufanya hivyo utekelezaji wa kauli mbiu ya kampeni hiyo ya ‘jiongeze tuwavushe salama’ itakuwa imetekelezwa vizuri.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...