Na Moshy Kiyungi,Tabora.
Bendi ya Kyauri Voice Orchestra ilivunja rekodi ya kudumu kwa kipindi kifupi katika ‘game’ la muziki licha ya kuwa amaarufu kwa upigaji wake.
Bendi hiyo ilikuwa na makao yake makuu katika baa ya Mpakani iliyokuwa Mwenge jijini Dar es Salaam. Kyauri Voice ilikuwa ikipiga muziki kwa mtindo wa ‘Mwendo wa Jongoo’
Waliporomosha vibao ‘matata’ sana vilivyowakuna baadhi ya washabiki na wapenzi wa muziki katika jiji hilo, vikiwemo vya ‘Bangungi ee Nakobelela’, Mwaka wa Watoto na Tondo ulitungwa na Mukumbule Lolembo ‘Parashi’.
Ilikuwa imesheheni wanamuziki wakubwa we
nye vipaji vikubwa katika muziki. Baadhi ya wanamuziki hao ni Monga Stanie aliyekuwa akicharaza gitaa la solo na kuimba, Khatibu Itetei aliyekuwa akipuliza saxophoni, Kabaa Belela aliyekuwa akiliungurumisha gitaa zito la besi na Kawele Mutimanwa kwenye gitaa la solo.
Katika safu ya uimbaji bendi hiyo ilikuwa na mtunzi na mwimbaji Mukumbule Lolembo ‘Parash’
Nguli huyo vilevile alijulikana kama Eugine, ambaye alijiunga katika bendi hiyo akitokea katika bendi ya Orchestra Bana Ngenge, iliyofanya ziara humu nchini mwishoni mwaka 1978, hatimaye ikavunjika.
Alikuwa Khatibu Itetei alipoibua ‘dili’ la kuanzisha bendi hiyo ya Kyauri Voice.Wakati wakiporomosha nyimbo, waalikuwa wa rap “Kata kata kata kata mwendo wa Jongooo pamoja na vumbi nyuma”.
Bendi hiyo licha ya kuwa na mtunzi na mwimbaji mahiri aliyepata sifa lukuki Barani Afrika, Moreno Batamba, alisambaratika baada ya kipindi kifupi mno.Moreno Batamba aliaga dunia mwaka 1993 akiwa nyumbani kwake huko Dandora estate, jijini Nairobi nchini Kenya.
Wakati wa uhai wake alitamba na nyimbo nyingi ukiwemo uliompa sifa ndefu wa ‘Pili Muswahili’.Wimbo wake wa mwisho alitunga kabla ya kifo chake ulikuwa wa ‘Vidonge sitaki’ wa mwaka 1983.
Sababu kubwa ya kusambaratika kwa bendi hiyo ilikuwa mmiliki wa bendi ya Kyauri Voice ni kutokuelewana na wanamuziki wake.Wanamuziki wa bendi hiyo ya Kyauri Voice, walikuwa ni raia toka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wakati huo Zaire.
Kwa kulikuwepo na bendi mbili Maquis du Zaire na Safari Soud (OSS) zilizokuwa na wanamuziki wengi toka huko DRC, baadhi ya wanamuziki hao walikwenda kujiunga katika benadi hizo.
Mwanamuziki Monga Stinie alikwenda kujiunga katika bendi ya Safari Sound, Batii Osie Senga, Labaa, mwanamuziki aliyejulikana kama Cobra na Biliumbu na wengine kadhaa.
Kawele Mutimanwa akachepukia katika mji wa Bujumbura nchi Burundi baadaye alirejea tena nchini humu akajiunga katika bendi za MK. Group na Tancut Alimasi. Hivi sasa Kawele amefanya makazi yake katika jiji la London nchini Uingereza.
Baada ya bendi ya Kyauri Voice kusambaratika wanamuziki wengine wakaenda kujiunga katika bendi ya Super Matimila, iliyokuwa ikiongozwa na Ramadhani Mtoro ‘Dk. Remmy Ongalla.
Dk.Remmy Ongala naye alizaliwa mwaka 1947 katika mkoa wa Kivu huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo mwaka 1947. Mukumbule alichukuliwa katika bendi ya Maquis du Zaire, iliyokuwa ikiporomosha muziki wake katika ukumbi wa White House, Ubungo jijini Dar es Salaam.
Parashi alichukuliwa ka minajiri ya kuziba pengo lililoaca wazi na Kikumbi Mwanza Mpango ‘King Kiki’ aliyekuwa amekwenda kujiunga katika bendi ya OSS.
Hapo Maquis, alijumuika na safu kamambe ya watunzi na waimbaji akina Mbuya Makonga ‘Adios’, Mutombo Lufungula ‘Audax’ na Abubakar Kasongo Mpinda ‘Clyaton’.
Wengine ni pamoja na Kasalo Kyanga na Tshimanga Kalala Assosa wakiongozwa na kiongozi wao Tshinyama Tshiayaza.Baada ya kipindi kifupi wakaenda kurekodi albamu yao katika studio ya RTD, wakati huo.
Katika albam hiyo kulikuwa na nyimbo za Kiongo, Maiga, Zoa Pondamali na nyingine nyingi.Albam hiyo hadi sasa ni miongoni mwa kazi zenye kiwango cha hali ya juu kulichoakuliwa wakati huo.
Maquis du Zaire katika albam hiyo, aliwatumia wanamuziki kujipanga katika uimbaji na jinsi walivyowatuamia wanamuziki wa Tanzania Mafumu Bilal ‘Bombenga’, Abdallah Kimeza walikuwa wakipuliza saxophone.
Mafumu Bilal yupo hai anamiliki bendi yake binfasi, Abdallah Kimeza alikwisha tangulia mbele za haki.Aidha wanamuziki Matei Joseph, Steven Kaigilila Mauffi, Majengo Bakari na mwimbaji Tabia Mwanjelwa nao waliungana na Wakongo hao.
Matei Joseph hivi sasa namiliki bendi yake ya African Minofu, Steven Kaigilila Mauffi, ni mcharazaji wa gitaa la rhythm katika bendi ya Mlimani Park, Majengo Bakari alikuwa katika bendi ya Shikamoo Jazz na Tabia Mwanjelwa aliachana na muziki baada ya kuolewa nchini Ujerumani.
Parashi miaka ya karibuni alikuwa jijini Mwanza akifayakazi ya muziki katika bendi ya Kamanyola, akishirikiana vema na mtuzi na mwimbaji Benno Villa Anthony na Mkuna Roy ‘Mukuna wa Mukuna’ hivi sasa ni marehemu.
Kama ambavyo baadhi ya wanamuziki hususan wa zamani, Parashi naye ametamka kuwa muziki wa dansi haujafa, ila ukosefu wa promosheni katika muziki wa dansi, ikiwemo kwa baadhi ya vituo vya redio kutokuthamini muziki huo pia makampuni yaliyopo hivi sasa imewapa kisogo.
Ni imani yake kuwa muziki huo unaweza kurejea katika nafasi yake iwapo utathaminiwa kama zamani hasa ikizingatiwa kuwa wataalamu wa muziki wa dansi bado wapo ambao wangeweza hata kuwafunza vijana wa sasa kupiga muziki.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...