Kauli ya mgeni njoo, mwenyeji apone imedhihirika baada ya ujio wa simu za Phantom kutoka TECNO mobile. Ni moja kati ya simu pendwa miongoni wa watumiaji wa simu za TECNO toka 2015. Ni lipi hasa inaifanya matoleo ya Phantom kuiteka soko?

Mara zote Phantom hua inatolewa kila mwaka ikiwa imeshiba specifications na features kali kuliko! Ilikua ikisemekana kwamba kwakua mwaka jana TECNO hawakutoa toleo la Phantom, kampuni hiyo ilikua inafanya utafiti na kujipanga kuleta simu ambayo itakua ipo vizuri kwenye kila sekta.

Tetesi hizo ziligundulika kua ni za kweli baada ya kampuni kuzindua simu hiyo mpya ya Phantom 9 mwezi huu huko nchini India. Uzinduzi huo ulienda sambamba na kampuni kutangaza kuongeza mkataba wa ushirikiano wao na klabu kubwa Uingereza ya Manchester City, pamoja na kubadili kauli mbiu yao kutoka “Experience more” kwenda “Expect More”, yaani ikimaanisha ‘tarajia zaidi’. 

Dhima kuu ya kauli hii ni kuwahakikishia watumiaji wa simu za TECNO juu ya ubora na uimara zaidi utakaoletwa na kumpuni hii pendwa nchini na kwenye bara kwa ujumla. Kwa sasa, TECNO inashika nafasi ya 5 Afrika kama kampuni ya simu pendwa.

Nisikuchoshe sana, hakika simu hii imekuja na muundo wa kipekee na mzuri zaidi wa kuvutia. Kamera tatu za nyuma, kamera ya mbele, kioo kikubwa na kizuri zaidi chenye muundo wa “dot notch” kwa juu pale katikati.

Tumekua tukiona makampuni mengi ya simu yakiondoa tundu la kuchomeka earphone; lakini hapa kwenye Phantom 9 TECNO wameona watuachie “earphone jack” ambayo ipo upande wa chini wa simu hiyo.

We unaona ni jambo gani limekuvutia sana kutoka toleo hili? Endelea kutufuatilia kwa ajili ya kupata sifa nyingine nyingi pamoja na maelezo ya undani kabisa kuhusiana na TECNO Phantom 9.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...