Leo tarehe 24/07/2019 Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) Organaizesheni ndg Pereira A. Silima ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu na Mlezi wa CCM Mikoa ya Katavi na Rukwa amekutana na viongozi wa dini zote katika Wilaya ya Sumbawanga mjini Mkoani Rukwa kwa lengo la kusikiliza changamoto zao na kuwakumbusha mchango wao katika ujenzi wa Taifa. 

Katika Mkutano huo, ndg Pereira amewaomba kuendelea kulinda na kutetea amani ya nchi kwa kuwa wao ndiyo walezi muhimu katika jambo hilo na kuwakumbusha umuhimu wa kufundisha vijana wanaopoteza maadili ili kuwarudisha katika maadili stahiki ya nchi yetu ya Tanzania. Pamoja na hayo, Viongozi hao wamepata nafasi ya kutoa ushauri, kuuliza maswali mbalimbali na kupatiwa majawabu kutoka kwa viongozi wa Chama na Serikali waliohudhuria. 

Ndg Pereira amewaomba kuendelea kuhubiri na kusimamia Umoja katika jamii zao, kutobaguana wala kutengana kwani binadamu wote ni sawa kama ambavyo imani ya Chama Cha Mapinduzi inasema katika Katiba yake na mwisho amewashukuru na kuwapongeza kwa kazi kubwa wanazozifanya katika kutoa mchango wa kulijenga Taifa. 


Leo tarehe 24/07/2019 ndg Pereira anaendelea na ziara yake ambapo anatarajiwa kuzungumza na viongozi wa Mashina, Matawi na Kata za CCM katika Wilaya ya Sumbawanga Mjini mkoani Rukwa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...