Mwenyekiti wa usalama Barabarani, Salim Abri akizungumza wakati wa uzinduzi ofisi ya madereva daladala.

Mwenyekiti wa usalama Barabarani
mkoa wa Iringa, Salim Abri akiwa katika picha ya pamoja na madereva
daladala wa manispaa ya Iringa
**************
NA DENIS MLOWE, IRINGA
MWENYEKITI wa kamati ya
Usalama Barabarani mkoa wa Iringa, Salim Abri, amewataka madereva
daladala kuzingatia sheria za usalama pindi wanapokuwa wakiendesha
daladala zao.
Akizungumza wakati wa
uzinduzi wa ofisi mpya ya madereva wa daladala manispaa ya Iringa, Abri
alisema kuwa ifike wakati madereva wafate sheria kuepukana na usumbufu
wa vyombo vya usalama.
Alisema kuwa imekuwa
kawaida ya madereva wa daladala kuvunja sheria kisha kuanza malalamiko
kwamba wanaonewa na polisi wa usalama Barabarani hali ambayo
imesababishwa na madereva kutofata sheria.
Abri ambaye pia ni mkurugenzi wa kampuni ya
usafirishaji ya Asas alisema kuwa kuna baadhi ya madereva wanaokiuka
taratibu za ushafirishaji ikiwemo kutofika mwisho wa vituo hali
inayoleta usumbufu kwa abiria.
Alisema madereva wanapaswa kufata sheria ikiwemo
kutoa tiketi kwa abiria lakini pia kuepuka kuwanyanyasa abiria kwa
kutotumia lugha mbaya kwa abiria ambao wamewapakia.
Aliongeza kuwa licha ya kufata sheria madereva
wametakiwa kuondokana na migomo isiyokuwa na maana kwa lengo la
kufikisha kilio chao katika mamlaka husika kwani kugoma sio njia ya
kutatua tatizo.
“Hivi unavyogoma mnajua kwamba wengine wanafurahia
Sana hali hiyo? Kumbukeni kuna njia nyingi za kufikisha ujumbe kwa
serikali endapo mnaona mambo hayapo sawa hivyo acheni tabia ya kugoma”
Alisema
Katika
uzinduzi huo Abri aliwachangia sh. Milioni kumi kwa ajili ya kufungua
Saccos ya madereva daladala na kuwataka kutumia vyema Saccos hiyo katika
kukuza uchumi.
Aliwataka
pia kuacha tabia ya kushabikia mambo ya siasa zisizo na faida kwao
ambazo haziwezi leta maendeleo kisa unafata mkumbo kutoka kwa watu
wengine.
Alisema
kuwa wanatakiwa kuangalia viongozi ambao wapo kwa ajili ya kuwaletea
maendeleo ambayo wanayataka na kukiamini chama cha Mapinduzi chenye nia
haswa ya kuwaletea maendeleo wananchi wake.
Kwa
upande wao madereva wa daladala kupitia katibu wao, Rashid Ayubu
waliomba mafunzo ya Mara kwa Mara ikiwezekana kila baada ya miezi Sita
kutokana na mabadiliko ya sheria ya mara kwa mara.
Ayubu
alisema kuwa umoja huo Una mpango wa kupata gari aina ya Kosta kwa
lengo la kuwaongezea kipato lenye thamani ya sh. Milioni 56 na kufungua
Saccos ya umoja huo.
Aidha
alisema kuwa changamoto kubwa wanayokumbana nayo ni baadhi ya barabara
zimekuwa chakavu na zinahitajika matengenezo makubwa na nyingine
kushindwa kuendelea na safari kutokana na kuvamiwa na bajaji na
bodaboda.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...