Na Said Mwishehe,Michuzi TV
MAOFISA wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali waliopo kwenye Maonesho ya Biashara ya 43 ya Kimataifa yanayoendelea viwanja vya Mwalim Nyerere maarufu Sabasaba jijini Dar es Salaam wameendelea kutoa maelezo ya kina kuhusu majukumu ya mamlaka hiyo.
Idadi ya wananchi wanaofika kwenye maonesho hayo wamekuwa wakienda katika banda la Mamlaka hiyo ambapo wengi wao wamekuwa wakitaka kufahamu zaidi kuhusu namna mtambo wa DNA unavyofanya kazi na wengine wakitaka kufahamu wanawezaje kutumia mamlaka hiyo katika shughuli zao za kila.
Akizunguza kwenye maonesho hayo ya biashara yanayoendelea katika viwanja hivyo Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Ubora wa Bidhaa Sabanitho Mtega ametumia nafasi hiyo kuelezea majukumu ya msingi yanayofanywa na mamlaka hiyo.
Ametaja baadhi ya majukumu hayo ni kufanya uchunguzi wa bidhaa mbalimbali kama vile vyakula, kufanya uchunguzi kwa ajili ya kusaidia vyombo vya ulinzi kufanya uchunguzi wa sampuli ambazo ni za makosa ya jinai kama vile dawa za kulevya, sampuli za sumu na aina nyingine za sampuli zote.
Pia Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali inadhamana ya kusimamia sheria namba tatu ya mwaka 2003 ambapo sheria hiyo pamoja na mambo mengine inasimamia utoaji wa vibali vya katika maeneo yote nchini ikiwemo kwenye viwanja vya ndege, mipakani na bandarini.
"Kwa kufanya hivyo inatuhakikishia kuwa Kemikali zote zinazoingizwa nchini hazileti madhara kwa mazingira na wakati huo huo kwa usalama wa nchi. Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali ndio iliyopewa dhamana kupitia sheria namba 8 ya mwaka 2016 kuwa matokeo yanayotolewa na mamlaka hiyo ndio ya mwisho na hayabishaniwi.
Pia ni chombo cha serikali ambacho kazi yake ni kuhakikisha vyombo vya maamuzi vinatapa matokeo ya uchunguzi ili kufanya maamuzi sahihi. "Tunawakaribisha wananchi kwenye banda la mamlaka yetu ili wapate maelezo ya kina kuhusu majukumu ya mamlaka hiyo.Pia kupata maelezo yatakayowasaidia kwenye maisha yao ya kila siku,"amesema.
Kuhusu uelewa , amesema kwa sasa wananchi wengi wanailewa mamlaka hiyo na wao wamekuwa wakitumia maonesho mbalimbali kutoa elimu kwa umma.Akizungumzia mtambo wa DNA amesema unafanya kazi nyingi zaidi ya kupima vinasaba vya kutambua uhalali wa mtoto na kwamba mtambo huo unatumika hata kupima sampuli za makosa ya jina, majanga ya moto, ndege, kubaini askari walipoata majanga.Pia kupima wanaohitaji kuwekewa figo ili kujua kama damu zao zinaendana.
Kwa upande wake Ofisa Masoko na Mawasiliano wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali Cletus Reuben Mnzava amesema wananchi wengi wanaofika kwenye banda lao kna mambo mengi wanapenda kufahamu.Baadhi ya mambo hayo ni kufahamu namna ambavyo maabara ya mkemia mkuu wa serikali inafanya kazi.Wengine wanataka kujua kuhusu mtambo wa DNA unatumika kupima sampuli za aina gani hasa ukiondoa kujua uhalali wa mtoto.
"Wapo baadhi ya wananchi ambao wanataka kufahamu kuhusu ubora wa bidhaa, pia wanaotaka kufahamu kuhusu usalama wa chakula na dawa ambazo wanazitumia."Wengine wanapenda kufahamu kuhusu uchunguzi wa sampuli ambazo zinafanywa na maabara ya mkemia mkuu.Kuna wajasiriamali ambao wao wakifika hapo wanataka kufahamu ni kwa namna gani maabara hiyo inaweza kutumika katika kuwafanya kuzalisha bidhaa zilizo bora.Wote wenye maswali tunawajibu na wanaridhika,"amesema Mnzava.
Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Ubora wa Bidhaa Sabanitho Mtega pichani kushoto akizungumza na mmoja wa wadau waliofika kwenye banda la Mkemia Mkuu kuusu majukumu ya msingi yanayofanywa na mamlaka hiyo.Ametaja baadhi ya majukumu hayo ni kufanya uchunguzi wa bidhaa mbalimbali kama vile vyakula, kufanya uchunguzi kwa ajili ya kusaidia vyombo vya ulinzi kufanya uchunguzi wa sampuli ambazo ni za makosa ya jinai kama vile dawa za kulevya, sampuli za sumu na aina nyingine za sampuli zote.Picha na Michuzi Jr.
Ofisa Masoko na Mawasiliano wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali Cletus Reuben Mnzava akizungumza na na baaadhi ya Wananchi waliofika kwenye banda hilo kufahamu mambo mbalimbali kuhusu mamlaka hiyo
MAOFISA wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali waliopo kwenye Maonesho ya Biashara ya 43 ya Kimataifa yanayoendelea viwanja vya Mwalim Nyerere maarufu Sabasaba jijini Dar es Salaam wameendelea kutoa maelezo ya kina kuhusu majukumu ya mamlaka hiyo.
Baadhi ya Wananchi wakiendelea kupata elimu na kufahamu mambo mbalimbali yahusuyo Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali kutoka kwa Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Ubora wa Bidhaa Sabanitho Mtega
Ofisa Masoko na Mawasiliano wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali Cletus Reuben Mnzava akizungumza na na baaadhi ya Wananchi waliofika kwenye banda hilo kufahamu mambo mbalimbali kuhusu mamlaka hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...