Na Andrew Chale, Zanzibbar
Watu zaidi ya 600 washiriki mbio za hisani za kuchangia malezi na elimu kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu kupitia Shirika la SOS Children’s Villages Zanzibar.
Awali mbio hizo zilizoanzia Ngome Kongwe majira ya asubuhi, washiriki hao kutoka maneo mbalimbali Zanzibar na nje ya Zanzibar wameweza kuanza na kumaliza huku wakipata medali za ushiriki.
Akizungumza na tuko Media, Mratibu wa mbio hizo David Lyamuya amesema kwa mwaka huu ni za mara ya kwanza na watu wadau wameonesha muitikio mkubwa wakiwemo wakimbiaji kutoka Arusha na maeneo mengine pamoja na wageni.
“Makampuni na mashirika ya hapa Zanzibar kwa ujumla wao wameweza kushiriki mbio hizi za kusaidia walio kwenye mazingira magumu. Tunawapongeza sana na watu wengine kwa kuchangia mbio kwani makusanyo yote ni kwa ajili ya watoto wetu.” Alieleza Lyamuya.
Lyamuya ameongeza kuwa, mbio hizo zinaongeza ufahamu wa malezi na ulinzi wa mtoto, kuimarisha mwili na pia kusaidia watoto na vijana ambao wamepoteza au ambao wapo katika hatari ya kupoteza malezi na uangalizi wa wazazi. Tunapenda kujivunia kwa kila mmoja aliyeshiriki kukimbia mbio hizi” alieleza Lyamuya.
Katika mbio hizo washiriki wote wameweza kukimbia mbio hizo na kumaliza ikiwemo mbio za Kilometa 5, Kilometa 10 na za Kilometa 21 zilizoanzia Ngome Kongwe na kuelekea SOS Mombasa kisha uwanja wa ndege, kilimani na kurejea kwenye viunga hivyo vya Ngome Kongwe.
Aidha, aliongeza kuwa SOS Children Village Zanzibar imeweza kujivunia kuweka mchango chanya katika ukuaji na ustawi wa watoto waishio kwenye mazingira hayo magumu zaidi kwani bado wanaweza kutimiza ndoto za kupitia fursa na elimu iliyo bora.
Shirika hilo la SOS Children’s Villages Zanzibar kwa visiwani hapa lipo Unguja na Pemba limejikita katika kutoa malezi na ulinzi wa watoto, kwa sasa shirika lina hudumia watoto 186 katika kijiji cha SOS kilichopo Mombasa Unguja na watoto na vijana 1920 waliopo katika miradi ya kuimarisha familia.
Shirika hilo linauzoefu wa zaidi ya miaka 27 katika melezi ya mtoto haswa wale walio kwenye mazingira magumu,kuiimarisha familia kwa ajili ya kuepusha kutojali na utelekezaji wa watoto na mambo mengine mengi.
Kwa sasa, shirika hilo pia inatekeleza miradi katika maeneo mbalimbali ya Pemba, Unguja, Mwanza, Arusha, Dare Salaam, Mufindi, Iringa, huku miradi iliyowafikia watoto na vijana 5,236 na kuboresha familia 1215.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...