MBUNGE wa kuteuliwa na Rais, Janeth Masaburi  ameeleza kusikitishwa kwake kwa baadhi ya vijana  wataifa  kukosa  maadili kwa kuwanenea maneno yasiyo ya maadili  wazee na viongozi jambo ambalo limesababisha wazee kupata maradhi ya moyo ama msongo wa mawazo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijiji Dar es Salaam Mbunge  Maburi , amesema  moja ya jambo linalochangia hilo ni pamoja na kukosa  upendo na maadili kutoka kwa wazazi wote wawili, kuiga mambo kutoka nchi za magharibi, wazazi kuwa dekeza watoto kupita kiasi, taama za haraka haraka na kutaka utukufu bila  kuwa na karama za mwenyezi Mungu, kukosa hofu ya Mungu, wazazi kutosimamia watoto katika misingi ya imani kwa kuwafundisha kuwa na upendo  na  kusamehe.

Aidha amewataka watanzani kuwa wamoja bila kugawanyika  katika kipindi hiki ambacho nchi inapiga hatua kimaendeleo na kusema kuwa katika miaka mitatu kuelekea minne ya utawala wa awamu ya tano  mwelekeo wa Rais Magufuli amekuwa mfano wa kuigwa kwani amejitolea kuwasaidia na kuwavusha watanzania kuwatoa katika zama za ujanja ujanja  (mission town) kuwa wachapa kazi.

Amesema kuwa miaka iliyopita  kulikuwa na shida kubwa katika upatikanaji wa huduma za maji, afya, elimu na ufisadi uliokithiri.

“Sisi sote tunao kula viapo kupitia vitabu vitakatifu Biblia na Quran tutambue kuwa viapo hivi vitatutafuna mbele za haki hivyo tusijidanganye  na kuwa jeuri kwa kuwa tuko hai tuanapumua  maslahi ya watu wa Mungu  ni ya kwanza kuliko nafsi zetu" ameeleza.

Amesema kuwa; "
 Rais Magufuli amekomesha ujangili, kaleta nidhamu kazini hasa katika ofisi za umma, heshima kwa wote hata mtaani tunaheshimiana, zamani ukimpeleka mtu Polisi baada ya kukutendea jambo baya  ubadilishiwa kesi wewe ndiyo unakuwa mshitakiwa" ameeleza.

Vilevile amesema kuwa serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Magufuli iwepiga vita dawa za kulevya kwa nguvu zake zote na kuwaokoa  vijana walikuwa wanaharibika kila siku na wauza unga wakambilia nchi za nje.


Amesema kuwa Rais Magufuli amekuwa jasiri wa kutetea wanachi na nchi yake kwa kupitia mikataba ya madini, na kusema kuwa chama cha Mapinduzi CCM kina hazina ya viongozi ambao  ni  mabalozi wa taifa.

“Tanzania yaleo siyo yajana na  CCM yaleo nibora kuliko  jana, Mwenyezi Mungu tunakuomba  mbariki rais wetu Dkt John Pombe Magufui  mpe ulinzi wako wote kwakuwa ana kutamka mbele ya mataifa  nawewe ulisema anaye nitamkana mbele ya mataifa, Magufuli amekutukuza mbele ya mataifa  kikasiku anaomba msaada  wako umlinde “Ameeleza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...