Anaandika Abdullatif Yunus wa Michuzi TV - Kagera.
Vijana na Wanachama wa Chama cha Mapinduzi Mkoani Kagera, wametakiwa kueleza kazi nzuri na kubwa iliyofanywa Nchi nzima na Uongozi wa awamu ya Tano chini ya Rais John Pombe Magufuli, Kagera ikiwa miongoni na kwamba hizi sio zama za propaganda.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Ndg. Kheri James wakati wa uzinduzi wa Programu ya Kagera ya Kijani mapema Julai 27, katika viwanja vya Hamugembe ndani ya Manispaa ya Bukoba, katika sherehe za Uzinduzi wa mkakati wa Kagera ya Kijani, zilizohudhuliwa na Wananchi, wanaharakati, makada na Viongozi wa CCM kutoka sehemu mbalimbali ndani na nje ya Mkoa wa Kagera.
Akihutubia maelfu ya wakazi wa Mkoa wa Kagera, katika hotuba yake iliyojaa ufafanuzi juu ya mambo makubwa yaliyofanywa na Mwenyekiti wa CCM Taifa Dkt. John Pombe Magufuli, Ndg. Kheri amesema Mhe.Rais Magufuli Amefanya mambo mengi kila sehemu ambayo mengi hayakuwezekana kwa kipindi cha nyuma lakini sasa yanaonekana dhahiri na kwa asiyeona basi afungue macho, kwani mambo makubwa yanakuja.
"Leo Vijana wote, akina mama wote, walemavu wote wana haki ya kupata fedha kutoka halmashauri zao, na fedha hizi zimefutiwa riba.......fungua macho" amesema Ndg. Kheri
Katika sherehe hizo Ndg. Kheri amepokea zaidi ya Vijana 50 walojiunga na CCM wakitokea vyama mbali mbali, waliokiri utendaji wa Dkt. John Pombe Magufuli, huku wajumbe, makada na wawakilishi wa CCM katika nyadhifa mbalimbali wameonesha utayari wa kutaka kufanya vizuri zaidi katika chaguzi ndogo zijazo za serikali za mitaa kwa kuhakikisha Chama cha Mapinduzi kinaibuka na ushindi mnono lilikiwa hasa ndilo lengo la Mkakati wa Kagera ya Kijani.
Hayo yanajiri wakati ambapo Taifa linajiandaa kwa uchaguzi wa serikali za mitaa, ikiwa kwa Kagera baadhi ya mitaa katika Wilaya inaongozwa na Vyama vya upinzani, huku Maandalizi zaidi yakielekezwa katika Jimbo la Bukoba Mjini linaloongozwa na Upinzani pia.
Pichani Ni Mwenyekiti wa Vijana CCM Taifa, Ndg. Kheri James akihutubia umati uliofurika katika sherehe za Uzinduzi wa Kagera ya Kijani, Mjini Bukoba.
Pichani Ndg. Kheri James M/kiti UVCCM Taifa akimshukuru Bi. Joan Kataraiya kwa ahadi ya Shilingi Milioni Moja ya Ukarabati wa Jengo la CCM Wilaya, katika harambee iliyofanywa na Kiongozi huyo.
Pichani ni wafuasi wa vyama vya upinzani waliorejea na wengine kujiunga na CCM rasmi baada ya kuridhika na utendaji kazi wa Awamu ya Tano.
Pichani Ndg. Kheri James M/kiti wa UVCCM Taifa akikabidhiwa kadi na bendera za wanachama wapya waliojiunga na CCM katika sherehe za uzinduzi wa Kagera ya Kijani.
Pichani Ndg. Joani Kataraiya akikabidhi bendera 400 kwa M/kiti wa UVCCM Taifa Ndg. Kheri James lengo likiwa kwenda kuongeza hamasa katika Chaguzi zijazo.
Kagera ya Kijani Tukutane Kaziini
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...