Anaandika Abdullatif Yunus wa Michuzi TV - Kagera.

Serikali kupitia Wizara ya Maji imesema haitakuwa tayari kuendelea kufanya kazi na Wakandarasi wasiokamilisha miradi ya Maji kwa wakati, badala yake wamekuwa hodari wa kuomba kulipwa pesa nyingi kabla ya utekelezaji wa Miradi husika.

Tamko hilo limetolewa na Waziri mwenye dhamana Profesa Makame Mabarawa Akiwa Wilayani Kyerwa akitokea Wilaya ya Karagwe katika ziara ya kikazi ambapo amesema kuwa, kwa miradi ya Maji Nchini ambayo inasua sua au imeshindwa kutoa Maji kama ilivyotarajiwa, Wakandarasi wataondolewa na Wizara yenyewe itahusika kutafuta Wakandarasi wapya wa kumalizia Miradi hiyo, tofauti na sasa ambapo Miradi inasimamiwa na Halmashauri au Mamlaka za Maji.

Akiwa Wilayani Kyerwa Mkoani Kagera, Waziri wa Maji Profesa Mbarawa ametembelea na kuijonea Ukarabati na Upanuzi wa Mradi wa Maji Mabira ambao ulianza kutekelezwa tangu Mwaka 2017 na Mkandarasi M/S Vumwe General Service and Supply Co.Ltd.

Mradi huo unaogharimu kiasi cha shilingi 586,747,480.00 unaosimamiwa na Halmashauri ya Wilaya Kyerwa, wenye lengo la kuhudumia wananchi wapatao 23,000 kufikia 2022, ulitakiwa kukamilika kwa sasa upo katika 80% na Mkandarasi tayari amelipwa zaidi ya Milioni 200.

Kufuatia hatua hiyo Waziri Mbarawa amemuagiza Mhandisi wa Mkoa pamoja na Uongozi wa Halmashauri kutolipa kiasi kilichosalia mpaka kazi yote itakapokamilika kwa wakati, kwani Makandarasi wengi wamekuwa wakishindwa kumaliza kazi kwa wakati na huku wakidai kulipwa kiasi kikubwa cha pesa. Waziri Mbarawa yupo Kagera kwa ziara ya kikazi ya kutembelea na Kukagua Miradi ya Maji, baada ya Kuhitimisha ziara hiyo Wilayani Kyerwa sasa Yupo Wilayani Ngara.
Pichani Waziri Wa Maji Profesa Makame Mbarawa akifungulia maji katika mradi wa Maji Mabira uliokamilika Kwa 80% unaoendelea kukarabatiwa na kupanuliwa ili kukidhi mahitaji ya Wananchi 23,000 ifikapo 2022.
Kazi ni moja kumtua Mama ndoo kichwani, kama anayoonekana Waziri wa Maji Profesa Mbarawa akifanya tendo hilo baada ya kujiridhisha na hatua ya mradi wa Mabira Nyamilima Wilayani Kyerwa ulipofikia.
Pichani Waziri wa Maji Profesa Mbarawa akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Mhe. Rashid Mwaimu, Mhandisi wa Maji Mkoa wa Kagera Avitus Exavery wakielekea kwenye Mradi wa Maji.
Pichani Waziri Mbarawa akionyesha moja kati ya Bei za vifaa vya mradi wa Maji kutoka Kiwandani, wakati akilinganisha na bei za mradi wa Maji Mabira uliopo Wilaya ya Kyerwa, alipotembelea mradi katika ziara yake.
Pichani ni tanki la Maji la Mradi wa Maji Mabira, unaosambazia Maji vijiji sita vya Rushe, Mabira, Omkagando, Kibimba, Makazi na Nyakatete wenye Gharama zaidi ya Shilingi Milioni 580, ukiendelelea kukarabatiwa na Kupanuliwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...