Na Said Mwishehe,Michuzi TV

MWALIMU wa madereva wa magari makubwa kutoka Chuo cha VETA-Kihonda mkoani Morogoro William Munuo amesema amebuni taa ambayo haitakuwa na ulazima tena kwa trafiki kuingia katikati kuongoza magari.

Kwa mujibu wa Munuo lengo si kuwaondoa askari wa usalama barabarani bali wanachotaka ni kuwapusha na ajali wanazozipata kwa baadhi yao kwa kugongwa na magari wakati wakiongoza na wakati mwingine kusababisha kupoteza maisha.

Akizungumza na Michuzi TV kwenye banda la VETA katika Maonesho ya Biashara ya 43 ya Kimataifa yanayoendelea jijini Dar es Salaam Munuo amesema taa hizo ambazo amebuni zitakwenda kusaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa tatizo la foleni na kubwa zaidi kuokoa maisha ya trafiki.Akifafanua zaidi Munuo amesema madereva wawapo barabarani kwa sehemu kubwa wanatumia lugha ya alama ikiwemo michoro, taa na askari wa usalama barabarani.

Hata hivyo, baada ya kuona askari hulazimika kuingia kati kati ya barabara kuongoza magari kutokana na taa zilizopo sasa kuwa za automatiki ndio maana amebuni aina mpya ya taa ambayo itaongozwa na binadamu kulingana na wingi wa magari.

"VETA-Kihonda tumeamua kubuni taa ambazo ni tofauti na hizi ambazo tumezoea kuziona barabarani. Zilizopo sasa ni taa ambazo zimeshawekwa muda maalum na haubadiliki, hivyo hulazimisha wakati mwingine trafiki kuingia katikati ya barabara kuongoza magari.

"Changamoto iliyopo dereva anaweza kuona taa ya kijani na akadhani ameruhusiwa kumbe wakati huo kuna askari anangoza kwa mikono.Hivyo taa ambazo nimebuni trafiki hataingia tena barabarani bali ataseti taa kulingana na foleni iliyopo kwa wakati huo,"amesema Munuo.

Amesisitiza kupitia taa ambazo amebuni askari atakaa pembeni ya barabara na ataendelea kuongoza magari kama kawaida kwa kutumia taa hizo.

"Tunahitaji kumsaidia askari wetu asigongwe na gari.Wasikae juani , lakini pia hatutaki wawe wanavuta hewa yenye moshi wa magari.Ukweli taa ikogongwa na kuharibika itatengenezwa nyingine lakini askari akigongwa ni hasara kwa nchi,"amesema.

Ameongeza kuwa tayari ubunifu wa taa hiyo ya kuongoza magari umeshapelekwa COSTECH ili kuuthibitisha na baada ya hapo wanaweza kuwapa TEMESA ambao ndio wanahusika na kufunga taa za barabarani na kufafanua kwa sasa bado hazijaanza kutumika.

Alipoulizwa iwapo taa hizo zitawadhibiti madereva bodaboda ambao wengi hawajali taa za barabarani, amesema ni ngumu kuwadhibiti lakini amewashauri wafuate sheria za usalama ili kuepuka ajali ambazo zinaepukika.
 Mwalimu wa madereva wa magari MAKUBWA kutoka VETA-Kihonda mkoani  Morogoro William Munuo akielezea aina ya taa ambazo ameobi kwa ajili ya kuongeza.magari ambazo ni tofauti  na taa zilizopo sasa
Mwalimu wa madereva wa magari makubwa kutoka VETA -Kihonda mkoani Morogoro William Munuo akionesha taa ambazo amebuni (pembeni kulia) ambazo ni maalum kuongeza magari bila trafiki kuingia barabarani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...