Na.Khadija seif, Michuzi tv

CHUO kikuu cha Mzumbe cha wanufaisha wajasiriamali wadogo na wakubwa kwa kuwapatia mafunzo na elimu jinsi ya kuboresha na kujiajiri katika biashara ili kufikia uchumi wa viwanda.

Akizungumza na Michuzi tv Makamu Mkuu wa chuo kikuu Mzumbe Pro.Lughano Kusiluka katika Maonyesho ya 43 ya kimataifa ya kibiashara (7'7 ) jijini Dar es salaam amesema wananchi watakaofika katika banda lao wataweza kupatiwa elimu ya ujasiriamali, namna ya kutafuta masoko pamoja na kuboresha 
biashara zao.

Hata hivyo Kusiluka ameeleza kuwa chuo hicho kinatoa mafunzo mbalimbali ambapo kimebobea kwenye utawala wa rasilimali watu,utawala wa kiuchumi ,utawala wa kibiashara, utawala wa umma.

"Wataalam mbalimbali katika kila eneo wapo kwenye banda kwa ajili ya kutoa elimu na ujuzi, maarifa pamoja na elimu ambavyo wameshapatiwa chuoni kwa vitendo,"

Pia ametoa wito kwa wale ambao watahitaji kujiunga na mwaka ujao wa masomo katika chuo hicho watapatiwa maelezo kwa kina jinsi ya kujiandikisha,kupata fomu pamoja na vigezo na masharti ya kujiunga.

Makamu Mkuu wa chuo hicho amesema imekua ni fursa ya kipekee kuwepo katika Maonyesho hayo kutokana na kukutana na wadau mbalimbali wakiwemo wa elimu pamoja na biashara na kutoa maelezo kwakina.


Kusiluka amefafanua kwa wahitimu ambao wameshapata mafunzo chuo cha hawajutii kupoteza miaka yao chuoni kwa sababu ya kupata faida katika kambi iliyopo chuoni hapo kwa wahitimum

"Tumeamua wanafunzi wanaohitimu waweze kukaa kambi ya ujasiriamali ili waweza kupata ujuzi na maarifa ya kujiajiri wao wenyewe na pia kutoa mawazo ya kiubunifu yatakayowawezesha watu kupata ajira kiurahisi zaidina kuboresha biashara kwani kwa sasa wahitimu wanapitia changamoto kubwa kuajiriwa kwenye makampuni ,"

Pia ametoa wito kwa wale ambao watahitaji kujiunga na mwaka mpya wa masomo katika chuo hicho watapatiwa maelezo kwa kina jinsi ya kujiandikisha pamoja na kupata fomu katika mikoa ya Dar es salaam, Morogoro na mikoa mingine.
Makamu Mkuu wa chuo cha Mzumbe prof.Lughano Kusiluka akishika bidhaa iliyotengenezwa na mwanafunzi wa chuo hicho aliyenufaika na mafunzo ya elimu ya ujasiriamali

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...