Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa Bodi ya wataalumu wa Manunuzi na Ugavi (PSPTB), Godfred Mbanyi akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kutangaza matokeo ya mitihani ya Bodi ya 18, pamoja na kutangaza rasmi nafasi ya usajili kwa ajili ya mitihani ya 19 ya Bodi hiyo itakayofanyika mwezi Novemba.

BODI ya wataalamu wa ununuzi na ugavi iimetangaza matokeo ya 18, pamoja na kutangaza rasmi nafasi ya usajili kwa ajili ya mitihani ya 19 ya bodi hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijiji Dar es Salaam Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa Bodi ya wataalumu wa ununuzi na Ugavi (PSPTB), Godfred Mbanyi amesema kuwa leo Julai mosi Bodi ya wakurugenzi imeidhinisha matokeo ya bodi ya 18 na kuwa rasmi.

Ameongeza kuwa mitihani hiyo ilifanywa katika vituo vitano nchini na zaidi ya watahiniwa 1400 walifanya mitihani huyo na watahiniwa zaidi ya 50 hawakuweza kufanya mitihani hiyo.

Aidha amesema kuwa Kuna baadhi ya watahiniwa ambao watarudia mitihani hiyo na kueleza kuwa somo la hesabu  linahitaji kutiliwa mkazo kwa kuwa ufaulu bado ni hafifu .

Vilevile amesema kuwa watahiniwa wawe na mawazo chanya na wao Kama Bodi watasimamia  vigezo vya ufaulu na kueleza kuwa uhidhinishaji wa matokeo hayo yanafungua milango ya kujisajili kwa mitihani ya 19 ya bodi hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari  Mbanyi  ameongeza kuwa kutakuwa na warsha maalumu pamoja kuwajengea uwezo katika kuandika tafiti na kujieleza kwa kuwa wanaandaliwa kuwa viongozi wa baadaye.

"kuwa ngazi zote za mafunzo zitazingatiwa na hiyo ni pamoja na kanuni na Sheria zote za mitihani " alisema Mbanyi .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...