Na Emanuel Madafa, Michuzi TV, Mbeya 

Raia Watatu wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mbeya wakikabiliwa na shitaka la uhujumu uchumi baada ya kukutwa wakisafirisha dhahabu gramu 1043.3 yenye thamani ya shilingi Milioni 98.5 kinyume cha sheria ya madini namba 14 ya mwaka 2010.

Washitakiwa hao Clive Rooney (62) raia wa Trish , na wenzake raia wa Uingereza Ross Stephan (34) na Robert Charles (59) wamekutwa na madini hayo katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Songwe Mkoani Mbeya Julai 3, mwaka huu.

Mbele ya Kaimu Hakimu Mkazi mfawidhi wa Mkoa Venance Mlingi washitakiwa hao hawakutakiwa kujibu chohote kutokanana mahakama hiyo kutokuwa na uwezo wa kusikiliza shauri hilo.

Upande wa Serikali umewakilishwa na mawakili watatu ambao ni Lugano Mwakilasa ,Jacqueline Nyantori na Ofmed Mtenga wakati upande wa utetezi ukiwa na mawakili watatu Boniphace Mwabukusi James Kyando na Kamru Habib.

Mwanasheria wa Serikali Jacqueline Nyantori ameileza Mahayana hiyo kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na kuiomba Mahakama iendelee na utaratibu.

Akitoa utetezi mbele ya Hakimu Venence Mlingi wakili wa utetezi Boniphace Mwabukusi ameiomba Mahakama kuwapatia dhamana wateja wake kwa madai kuwa mshitakiwa wa kwanza ambaye ni Clive Rooney (62) anasumbuliwa na Ugonjwa haukutajwa nakwamba anatumia dawa maalumu.

Hata hivyo ombi hilo lilipingwa na wakili wa serikali Jacqueline Nyantori na kudai kuwa Ugonjwa huo utatibiwa kwa mujibu wa sheria ya nchi akiwa gerezani.Washitakiwa hao wote watatu wamerejeshwa mahabusu mpaka Julai 22 mwaka huu .






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...