Na Humphrey Shao, Michuzi Tv, Mwanza
Rais Dk. John Magufuli anatarajia kuzindua rasmi Hifadhi ya Taifa ya Burigi Chato Julai 9 mwaka huu.
 Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Maliasili na Utalii Dk. Hamis Kigwangala wakati wa ufunguzi wa mkutano wa  mwaka 2019 wa TANAPA  kwa Wahariri na Wanahabari Waandamizi uliofanyika jijini Mwanza.

Awali hifadhi ya taifa ya Burigi  CHATO ilikua pori la akiba lililojulikana kwa jina la Burigi kabla ya kupandishwa hadhi na TANAPA.

Mkutano huo umebeba kauli mbiu "Miaka 60 ya Tanapa kuimarisha uhifadhi pamoja na kupanua wigo na fursa za Utalii Kusini Magharibi na kaskazini Magharibi mwa Tanzania.

Aidha Waziri Kigwangala amesema kuwa Uhifadhi wa rasilimali za misitu na vyanzo vya maji pamoja na wanyamapori ni kitu pekee ambacho kinaweza kuendelea kutusaidia kuwa na uchumi imara hapo mbeleni.

Ametaja kuwa sekta ya Utalii uchangia zaidi ya asilimia 17.6 katika pato la Taifa na ajira za moja kwa moja ni laki sita huku watu zaidi ya milioni mbili wakiwa wameajiriwa katika mfumo usio rasmi.

Anasema kuwa uhifadhi umekuwa  na faida kubwa Sana kwa watanzania sio kwa kuleta kipato tu bali hata katika mfumo wa ecolojia ya maisha ya binadamu kwani sisi tunapata oxygen safi kutokana na uhifadhi mzuri wa misitu.
 Waziri wa Maliasili na Utalii,Dr Hamisi Kigwangala akizungumza na wahariri pamoja na waandishi waandamizi katika mkutano wa mwaka unaofanyika jijini Mwanza
 Kamishna wa uhifadhi-Tanapa, Dkt Allan Kijazi akitoa somo juu ya mabadiliko kutoka mfumo wa kiraia kwenda jeshi usu
Kamishna Msaidizi  Mwandamizi wa uhifadhi  Mawasiliano Tanapa  Pascal Shelutete akitoa utambulisho wa wanahabari kwa Waziri.
 Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongela akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri Kigwangala kuzungumza na Wahariri.
 Mhariri wa gazeti la Jamhuri Jackton Manyerere akichangia mada katika mkutano huo
 Baadhi ya Wahariri wakifatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa katika mkutano huo
Waziri Dr Hamisi Kigwangala akiwa katika picha ya pamoja na washiriki

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...