Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii.
BAADA ya Msanii wa filamu nchini, Wema Sepetu mwezi uliopita kufutiwa dhamana na kukaa rumande kwa siku saba, kwa kukiuka masharti ya dhamana na baadae kurudishiwa dhamana yake, leo tena kwa mara nyingine amezua tafrani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kufuatia kugoma kukamatwa baada ya kesi yake kufutwa.
Wema ambae anakabiliwa mahakamani hapo kwa makosa ya kusambaza video za ngono katika mitandao ya kijamii kupitia simu yake ya kiganjani, amegoma kukamatwa na polisi baada ya mahakama hiyo kumwachia huru chini ya kifungu cha sheria cha 225 na kisha kumkamata tena na kumuweka mahabusu.
Baada ya kuachiwa huru leo Julai 4.2019 Wema alitoka nje na wakati askari wakimkamata kwa nguvu, Wema aligoma kukamatwa hali iliyosababisha mvutano kwa muda kati ya askari na mawakili wanaomtetea, Albert Msando na Reuben Simwanza.
Hata hivyo, askari walifanikiwa kumkamata msanii huyo ambae pia ni Miss Tanzania mwaka 2006.
Hatua hiyo imefikwa baada ya wakili wa Serikali, Glory Mwenda kudai mahakamani hapo kwa hana shahidi kwani shahidi aliyemuandaa, Koplo Safi kudai ni mgonjwa.
Hata hivyo, hoja hiyo imepingwa na Wakili Msando kwa madai kwamba haina mashiko kwani mahakama ilishatoa ahirisho la mwisho hivyo hawawezi kuahirisha tena. Amedai kesi hiyo ipo mahakamani hapo kwa zaidi ya siku 60 na upande wa mashtaka wameshindwa kuleta mashahidi, "tunaomba chini ya kifungu namba 225(5) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai sura ya 20 mshtakiwa aachiwe huru".
Kauli hiyo ilipingwa na wakili Mwenda akidai sheria ya siku 60 inatumika pale tu ambapo upelelezi haujakamilika hivyo aliomba kesi iahirishwe.
Hakimu Kasonde, alikubaliana na maombi ya upande wa utetezi kuwa sheria hiyo inatumika wakati wowote hata hivyo alimuachia huru mshtakiwa Wema chini ya kifungu hicho cha sheria



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...