
Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
BENI Caid Essebsi ambaye ni Rais wa kwanza kuchaguliwa kidemokrasia nchini Tunisia amefariki leo alfajiri akiwa na miaka 92 katika hospitali ya jeshi nchini humo.
Taarifa iliyotolewa na kijana wa Rais huyo Hafedh Caid ameeleza kuwa baba yake Essebsi amefariki dunia leo alfajiri na hiyo ni baada ya kulazwa mara kwa mara katika hospitali hiyo kuanzia mwisho wa mwezi Juni na hadi leo mambo hayakwenda sawa.
Kabla ya kushika nafasi hiyo Essebsi aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali zikiwemo waziri mkuu mwaka 2011 na baadaye kuwa Rais wa nchi hiyo.Pia amewahi kushinda tuzo ya amani ya Nobel mwaka 2015 na hakutangaza nia ya kugombea nafasi ya kiti hicho katika uchaguzi utakaofanyika Novemba mwaka huu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...