
Amesema mkutano huo umeadhimia kuwaita viongozi hao ili kuja kutatua mgogoro uliopo ndani ya shule ya Msingi Mtoni Kijichi baina ya Kamati ya Wazazi, Mwalimu na diwani wa kijichi.
Amesema, diwani wa Kijichi, Eliasa Mtarawanje pia anidaiwa kuwatishia wazazi wa shule hiyo kupitia kwa Katibu wa Kamati ya Wazazi, Mathias Balijuza kuwa endapo watafanya mkutano shuleni hapo, atawafunga.
Akizungumza katika mkutano uliofanyika hivi karibuni shuleni hapo katika chumba cha darasa la VII A, Bulijuza amesema kuwa alitishiwa kufungwa na diwani huyo, baada ya kutaka kuwatangazia wanafunzi wa darasa la saba wa shule hiyo, wawaambie wazazi wao waje kwenye kikao.
"Alinitishia, Balijuza nitakufunga, nitakufunga wewe unataka kuleta fujo kwenye eneo la shule, angalia nitakufunga, picha hiyo ilinichanganya ikabidi niwapatie wazazi taarifa ya mkutano kupitia ujumbe wa simu" amesema Balijuza.
Amesema, kufuatia tishio hilo, baadhi ya wazazi walihofia kufika kwenye kikao hicho kwa sababu mimi nilikwenda kutoa taarifa kwa niaba ya wazazi wote,"
Naye Mwenyekiti wa Mtaa wa Butiama, Kata ya Kijichi, Haji Mgaya amesema amepata mualiko kupitia Kamati ya Shule kwa ajili ya kwenda kuangalia mchakato mzima wa elimu bure, lakini alipofika katika mkutano huo alikutana na changamoto nyingi ikiwemo ya Mwalimu Mkuu kushushwa cheo na madarasa yanayotumikaga kufanyia mikutano yamefungwa.
" Niwatoe hofu wazazi, sisi na Kamati ya wazazi tunasimamia sheria, hakuna taasisi yoyote ya kipolisi inayoweza kufanya jambo kinyume na taratibu na sisi tupo kwenye miongozo ndiyo maana tunaalika watu wenye sifa kuja kutoa maamuzi
Kuhusiana na kufungwa kwa milango la madarasa, Kaimu Mkuu wa shule hiyo, Twaha Kifunde alisema madarasa hayo yalifungwa kama kawaida na walinzi, kwa sababu hakukuwa na mkutano rasmi shuleni hapo na mtu wa kwanza kutangaza mkutano ni Mwalimu Mkuu.
"Hakuna aliyeniambia nimfungulie vyumba vya madarasa nikakataa na hii taarifa ya kuwa mimi nipewa maelekezo na diwani ya kukataza mkutano usifanyike shuleni hapa si za kweli, kwa sababu kuna utaratibu wa kufanya mikutano," alisema Mwalimu Kifunde
Naye Diwani Mtarawanje akijibu tuhuma hizo alisema hayo ni mambo ya kisiasa na kututaka tuachanenayo, kwa sababu yeye anasimamia Serikali kutokuchangisha wazazi michango ya shule kwa sababu, Serikali inatoa elimu bure.
"Haya mambo sitaki kuyasikia, sisi tunasimamia Serikali kutokuchangisha michango, mambo ya kupigiana pigiana simu sio, waache na tuhuma zao.Tuhuma zao zingine ni zipi? achana nazo hizo habari, mambo ya kisiasa hayo achana nayo," alisema Diwani Mtarawanje
Hayo yote yametokana na kikao cha wazazi kilichokaa kupitisha maadhimio kuwa kila mzazi mwenye mtoto wa darasa la sababu achangie Sh 8,000 kwa ajili ya masomo ya ziada, ambapo badae Mwalimu Munisi alishushwa daraja na kuwa Mwalimu wa kawaida kwa madai kuwa yeye ndiye alichangisha michango h
Amesema mchanganuo wa fedha hiyo ni kwamba , Sh 10,000 ni ya chakula cha mchana kwa wanafunzi hao, ambapo sahani ya chakula kwa siku ni sh 500 na Sh 5000 iliyobaki ni kwa ajili ya gharama ya uchapishaji wa mitihani ya masomo matano ambayo yatakuwa yanafanyika kila jumamosi ya wiki.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...