Moureen Rogath, Kasulu.

Serikali imesema iko mbioni kuzima umeme wa kutumia mashine mkoani Kigoma ifikapo 2020, na kuunganisha na umeme wa gridi ya Taifa ambao utakidhi mahitaji ya wananchi mkoani humo.

Akizungumza Naibu waziri wa Nishati Subira Mgalu wakati akiwasha umeme katika kijiji cha Shunga wilayani hapa, amesema serikali imejipanga na lengo ni kuhakikisha kila mtanzania anafikiwa na umeme. 

Amesema katika kutimiza dhamira hiyo tayari ujenzi wa msongo wa umeme 132 KV kutoka Tabora Urambo hadi Kigoma umeanza na kwamba fedha kwaajili ya kukamilisha kazi hiyo ipo tayari. 

"Lengo ni kuwa na umeme wa uhakika wa kukidhi mahitaji ya wananchi mkoa wa Kigoma kwani umeme unaozalishwa kwa sasa wa kutumia mashine ya mafuta hautoshelezi mahitaji na kupunguza gharama za uendeshaji. 

Amelitaka shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), kuwasimamia wakandarasi kuhakikisha wanafanya kazi kulingana na mikataba yao ikiwemo kutowatoza fedha zisizo rasmi ili kuwaunganishia umeme. 

"Kwa upande wa vijijini gharama za kuungansihwa kwa umeme uwe wa REA au Tanesco ni Sh. 27,000 kwa wote na kwamba wananchi hawatakiwi kutozwa zaidi ya kiasi hicho cha fedha," alisema Naibu waziri. 

Mkuu wa wilaya ya Kasulu Simon Annange alisema, wilaya hiyo ni moja ya wilaya yenye shughuli nyingi za kiuchumi lakini pamoja na maswala ya kiusalama kutokana na wilaya hiyo kupakana na nchi jirani ya Burundi.

Mkazi wa Kijiji hicho Faustina Pyeni mbali na kuishukuru serikali, alisema wao pia wanawajibu wa kuhakikisha wanafanya shughuli za uzalishaji mali katika kukuza uchumi wao baada ya kupata nishati hiyo. 

Naibu waziri huyo aliwasha umeme wa REA awamu ya pili katika kijiji cha Ruhita, pamoja na kukagua shughuli za zinazoendelea katika kikosi cha jeshi la kujenga taifa (jkt),mtabila.
Wanafunzi walio hitimu kidato cha sita na kupita jeshini kwa mujibu wa sheria katika kikosi cha jeshi la kujenga Taifa (jkt )wakitumbwiza mbele ya naibu waziri wa nishati Subira Mgalu wakati alipotembelea kikosi hapo kuangalia shughuli za uwekezaji umeme katika kambi hiyo.
Baadhi ya Wananchi wakifuatilia mkutano huo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...