MCHANGO WA MRADI WA SERIKALI WA EP4R - Shule ya Msingi Chimati iliyopo Kata ya Makojo imepokea kiasi cha Shillingi Million 12.5 kutoka kwenye MRADI huo wa Serikali na Wafadhili wake.
Fedha hizo (Tsh 12.5M) zimetolewa kwa ajili ya UPAUAJI na UKARABATI wa Vyumba vya Madarasa shuleni hapo.
Shule ya Msingi CHIMATI ina jumla ya Wanafunzi 437, Vyumba vya Madarasa vilipo ni vitatu (3), Mahitaji ni Vyumba vya Madarasa kumi (10), kwa hiyo WAPO Wanafunzi wanaosomea nje chini ya MITI. Kwa hali hiyo MRUNDIKANO ni mkubwa na Chumba kimoja cha Darasa kinachukua Wanafunzi kati ya 37 na 87.
Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Mwalimu Michael Hasunga ameeleza kwamba kwa sasa Shule ina MABOMA Matatu (3) na Ofisi moja (1) ambayo yakikamilika yatapunguza adha hizi, yaani mrundikano madarasani na kusomea chini ya miti.
Mwenyekiti Kijiji cha Chimati, Ndugu Masinde Bwire, ameeleza kwa namna ambavyo wameendelea kushawishi Wananchi kuhusu ukamilishaji wa Vyumba vya Madarasa. Wananchi wamekubali kuchangia NGUVUKAZI zao na Fedha taslimu Shillingi 5,000 (elfu tano) kutoka kila KAYA.
Aidha Mwenyekiti huyo, kwa niaba ya Wananchi wa Kijiji cha Chimati, amewashukuru WANANCHI wake na WADAU mbalimbali waliofanikisha ujenzi huo ikiwa ni pamoja na Mbunge wa Jimbo, Profesa Sospeter Muhongo ambae AMECHANGIA SARUJI MIFUKO 110, Madawati na Vitabu vingi.
MFUKO wa JIMBO umechangia MABATI 54. Vilevile Ndugu Beredy Maregesi amechangia Shilingi LAKI TANO (Laki 5).
Pichani ni Upauaji wa Vyumba vya Madarasa na Ofisi kwenye Shule ya Msingi Chimati iliyoko Kata ya Makojo.




Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...