WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewakaribisha wawekezaji na wafanyabiashara mbalimbali kutoka Misri ikiwemo kampuni ya Cairo for Investment and Development inayoshughulika na usimamizi wa kiwanda cha ngozi waje kuwekeza nchini Tanzania.

Ametoa kauli hiyo jana (Jumanne, Julai 9, 2019) alipotembelea kiwanda kikubwa cha ngozi cha Robbiki kilichoko katika mkoa wa Sharkianchini Misri, ambapo alitumia fursa hiyo kuwakaribisha wawekezaji hao waje wawekeze nchini kwani kuna malighafi za kutosha.

Waziri Mkuu ambaje jana alikuwa katika siku ya pili ya ziara yake ya kikazi nchini Misri alisema Tanzania inamifugo mingi hivyo inahitaji wawekezaji watakaojenga viwanda vya kuchakata bidhaa mbalimbali zitokanazo na mifugo hiyo ikiwemo ngozi.

Alisema Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli imeboresha mazingira ya biashara na ya uwekezaji pamoja na kusimamia uwajibikaji kwa watumishi wa umma, hivyo Tanzania ni mahali bora na salama kwa wawekezaji na wafanyabiashara.

Kwa upande wake,Mwenyekiti wa Kampuni ya Cairo for Investment and Development ya nchini Misri, ambayo inasimamia kiwanda cha ngozi cha Robbiki, Yasser Mohamed Ahmed Al Maghraby alisema kiwanda hicho kinauhitaji mkubwa wa ngozi kutoka Tanzania.

Awali, Waziri Mkuu alitembelea mradi mkubwa wa mabwawa ya kufugia samaki, mradi wa upanuzi wa awamu ya pili ya mfereji wa suez canal, ambapo aliipongeza Serikali ya Misri kwa ujenzi wa mradi huo mkubwa kwa kutumia fedha za ndani (Dola bilioni 8.2).
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Watanzania waishiyo nchini Egypt, katika hoteli ya Almasa, mjini Cairo, Julai 9, 2019.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akipokea picha ya Rais Magufuli, iliyochorwa na Binti wa Dereva wa Ubalozi wa Tanzania nchini Misri, Hadeer Mohamed, kwenye mkutano na Watanzania waishiyo nchini Egypt, uliyofanyika katika hoteli ya Almasa, mjini Cairo, Julai 9.2019. Katikati ni Balozi wa Tanzania nchini Misri, Meja Jenerali Mstaafu, Issa Suleiman. 
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiangalia bidhaa ya ngozi, wakati alipotembelea kiwanda kikubwa cha ngozi cha Robbiki, kilichopo katika mkoa wa Sharkia, nchini Misri, Julai 9.2019.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Mwenyekiti wa Mamlaka ya Mfereji wa Suez Canal, Admiral Mohab, wakati alipotembelea mfereji huo mpya nchini Misri, Julai 9.2019. 
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akipokea zawadi ya ngao, kutoka kwa Mwenyekiti wa Mamlaka ya Mfereji wa Suez Canal, Admiral Mohab, wakati alipotembelea mfereji huo mpya nchini Misri, Julai 9.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Mwenyekiti wa Mamlaka ya Mfereji wa Suez Canal, Admiral Mohab, wakati alipotembelea mfereji huo mpya nchini Misri, Julai 9.2019. 
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwa kwenye boti,wakati alipotembelea mfereji wa Suez Canal, katika mji wa Ismailia, Misri Julai 9.2019. 



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...