Na Charles James, Michuzi TV

MBUNGE wa Jimbo la Dodoma Mjini na Naibu Waziri wa Kazi, Vijana, Ajira n Mh Anthony Mavunde amewasihi wananchi wa eneo la Mjimwema kata ya Chang'ombe Jijini Dodoma kuendelea kuwa watulivu kwani mgogoro wa ardhi unaowakabili kwa muda mrefu umefanyiwa kazi na muda sio mrefu wataona matokeo yake.

Mh Mavunde ameyasema hayo Julai 9, mwaka huu wakati wa hafla ya uzinduzi wa Shina la wakereketwa wa Chama cha Mapinduzi (CCM) iliyofanyika katika eneo la Soko la Mavunde-Chang'ombe.

Mbunge huyo amesema katika utatuzi wa mgogoro huo hadi sasa tayari kuna hatua kadhaa zimekwisha chukuliwa tofauti na ilivyokuwa hapo awali.

"Hivi sasa Mkuu wetu wa Mkoa ameunda ile kamati yake na ilirudi hapa kutoa taarifa na baadhi ya mambo yanaendelea naomba tusubiri tukamilishe zoezi hili kama kutakuwa na mapungufu yatakayojitokeza kama viongozi wenu tupo tutasaidia kuweza kutatua lakini cha msingi ni kwamba ile kero kubwa tayari hatua zimeanza kuchukuliwa" Amesema Mavunde.

Kuhusu mikopo Mh Mavunde amewaahidi wananchi na wafanyabishara wa kata hiyo kuwa atashirikiana na viongozi wenzake ili kuwasaidia wale wote wenye vikundi kuweza kupata mikopo inayotolewa na Halmashauri ya Jiji pamoja na mifuko mingine ya uwezeshaji wananchi kiuchumi.

"Sasa hivi Jiji lenu linatoa mikopo ya hadi Shilingi Milioni kumi kwa kikundi niwaombe wafanyabiashara kama mna utaratibu wenu wa vikundi mmeuweka niletee ili niweze kuwasaidia kupata mikopo kupitia fedha hizi za Halmashauri ambazo vijana na akina mama wengi wamenufaika nazo "Amesema Mhe Mavunde.

Aidha katika ufunguzi wa Shina hilo Mh.Mavunde pamoja na kuelezea miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali katika Jiji hilo pia ameahidi kuweka uzio wa kuzuia jua katika Soko la Chang'ombe,Mipira na Jezi katika Timu ya shina pamoja na kuchangia kiasi cha Shilingi Milioni Moja kwa ajili ya kutunisha mfuko wa shina.

Wakizungumza katika tukio hilo baadhi ya wananchi wamekiri Mbunge wao kuwa na mchango mkubwa katika kuwaletea maendeleo katika kata yao na kumshukuru kwa mchango wa mabati na gharama za ufundi wa ujenzi wa soko na kuahidi kushirikiana nae katika kuwaletea wananchi maendeleo.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...