Na Charles James, MICHUZI TV

TAASISI ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini (TAKUKURU) mkoa wa Dodoma inatarajia kuwafikisha mahakamani watu saba wanaotuhumiwa kujihusisha na vitendo vya kuomba na kupokea rushwa kinyume na kifungu cha sheria namba 11 ya mwaka 2007.

Moja ya watuhumiwa waliokamatwa ni mfanyabiashara Bahadur Hirji (68) mkazi wa mtaa wa Tembo Kata ya madukani jijini Dodoma na mwanae Nahid Bahadur (33) mhasibu wa Victory Bookshop kwa kosa la kuahidi kumpa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Mhe Patrobas Katambi sh mil 1.2 ili asifuatilie mapungufu katika utekelezaji wa amri ya Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya ya Dodoma kukazia hukumu iliowasilishwa kwake.

Akizungunza na waandishi wa habari Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Dodoma Sosthenes Kibwengo alisema baada ya TAKUKURU kupata taarifa ya watuhumiwa kutoa fedha hiyo ya kishawishi kwa Mkuu wa wilaya walianza kuwafuatilia na kufanikiwa kuwakamata Julai 27 katika hoteli ya Royal village iliopo Area D baada ya mtuhumiwa Nahid kumkabidhi Mkuu wa wilaya rushwa hiyo.

Kibwengo alisema ukiacha watuhumiwa hao pia wamemkamata Omary Mtauka ambae ni msaidizi wa mtendaji wa Kata ya Makutupora iliopo jijini Dodoma baada ya kupokea rushwa ya sh 110,000 kutoka kwa Mzee Paulo Mawope (78) mkazi wa Chilungule Kata ya Makutupora ili wamalize tuhuma dhidi ya kugombana na jirani zake zilizowasilishwa na Mtendaji wa mtaa na badae ofisini kwake.

"Awali tulipokea taarifa kutoka kwa mjukuu wake kwamba amepigiwa simu na mtendaji wa Kata ya Makutupora uchunguzi watu uliweza kuthibitisha juu ya uwepo wa tukio hilo,na mtuhumiwa kujifanya ni mtendaji wa Kata hiyo," alisema Kibwengo.

Aidha alisema TAKUKURU inamshikilia Stanley Motambi(34) ambayo ni mtendaji wa Kijiji cha Matumbulu kilichopo Kata hiyo kwa kosa la kuomba na kupokea rushwa ya sh 65,000kinyume na taratibu za kiutendaji kutoka kwa Wilfred Mtundu ambaye alikuwa na shauri la mgigoro wa Ardhi mbele ya mtendaji wa kijiji kama kishawishi ili askilize shauri hilo.

Alisema baada ya kupata taarifa hiyo walifanya uchunguzi na kuthibitisha mtuhumiwa hiyo alitenda kosa hilo Junior tatu mwaka huu.

Aliwataka wengine waliokamatwa na vitendo hivyo vya rushwa ni Venance Mayo (34) na Sultan Rusheke (33) ambalo ni walimu wa sekondari ya viwandani iliopo jijini Dodoma ambalo waliomba fedha hiyo ili wampatie cheti cha utambulisho wa kusoma shule hiyo (leaving certificate).

Mtoa taarifa ambaye alikuwa Mwanafunzi wa shule hiyo alihitaji cheti hiko kwa ajili ya kuomba kozi fupi katika taasisi Moja ndipo akaenda shuleni hapo.

Alisema taarifa hiyo ikiwafikia TAKUKURU Julai 26 na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa Mayo akiwa kwenye Bajaji yenye namba MC686BHK ilioegeshwa kwenye uzio wa shule hiyo baada ya kupokea hongo hiyo na kumkabidhi muhusika cheti huku akiwa na muhuri wa Mkuu wa shule na kugonga kwenye cheti,kabla hajaondoka ndio alikamatwa ikiwemo Rusheke pia kwa sababu amehusika kutoa.

Mtuhumiwa Mwingine aliyekamatwa na ni Abdulhakim Kabunga (26) ambaye ni mtumushi wa muda wa mamlaka ya vitambulisho nchini (NIDA) Dodoma ambayo alikamatwa Julai 27 baada ya TAKUKURU kupata taarifa ya kwamba amepokea rushwa ya sh 30,000 kutoka kwa mtu mmoja aliyekuwa akihitaji kitambulisho cha taifa ili amsaidie kuipata haraka.

Alisema baada ya kuhojiwa mtuhumiwa huyo amekiri kuhusika na kitendo hiko huku taasisi hiyo ikiwakumbusha watu wanaofuatilia vitambulisho vya NIDA zoezi hilo utilewa bure na iwapo watatakiwa kutoa rushwa ili wahudumiwe wanatakiwa kutoa taarifa TAKUKURU.

Pia wanaendelea kuwakumbusha watumishi wa umma na wakazi wa Dodoma kwa ujumla kuzingatia maadiki ya utumishi ili kujiepusha na vitendo hivyo kwani vinaminya haki za wananchi.
Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Dodoma Sosthenes Kibwengo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...