Mkuu
wa Mkoa wa Dar Es Salaam Paul Makonda, leo Julai 29 amezindua kampeni
ya tano ya usafi yenye lengo la kuendeleza kufanya usafi wa jiji Dar es
Salaam ikiwa ni hatua za maandalizi ya kupokea ugeni wa viongozi wa
Umoja wa Nchi zilizo Kusini Mwa Afrika (SADC).
Akizungumza
na waandishi wa Habari Julai 29/2019 katika uzinduzi Kampeni ya Usafi
katika Uwanja wa Ndege Terminal I,Makonda amesema lengo kubwa ni kuweka
Jiji Safi huku akizitaka Taasisi zote za Serikali kuhakikisha kwamba
zinakuwa na watu wao wa usafi katika maeneo yao ya kazi.
Makonda
amesema pamoja na kuweka Jiji la Dar es Salaam kuwa safi ni kuonyesha
ubora wa wananchi wa jiji hilo na mikoa mingine ifanye hivyo na wakija
wajifunze vitu vingine ikiwemo usafi kutokana na kuwepo Marais 16 katika
mkutano wa SADC.
Amesema kuwa Mkoa wa Dar Es Salaam unachangamoto ya usafi hivyo ni vyema wakajenga utamaduni wa kufanya usafi Mara kwa Mara.
"Nataka
kuwaambia tu kwamba nimemsikia Mratibu wa kila Taasisi ya Serikali
katika mkoa wangu iwe na watu wa usafi" Amesema RC Makonda.Amesema ugeni
wa SADC ni heshima kwa Rais Dkt John Magufuli na Mkoa wa Dar Es Salaam
kwa ujumla hivyo lazima Jiji liwe safi wakati wa kuwapokea wageni pia
usafi huo uwe endelevu.
Katika
hotuba yake Makonda amewataka wakazi wa Dar Es Salaam, kuzingatia usafi
na kupiga marufuku mtu yoyote kufika mjini kama hajafanya usafi wa
mwili wake ikiwemo kuoga, kufua na kupiga pasi nguo zake.
“Tabia
ya kuja mjini hujafua, hujaoga usitutie aibu kama umezoea kuja mjini
hujaoga wala kufua nguo baki nyumbani walau huu mwezi wa nane uishe,
tunataka sio usafi tu wa mazingira, usafi pia wa wananchi wetu, watu
wamejaa chawa tu hapa”. Amesema.
“Ule
utaratibu wetu wa Lugalo tunauanza rasmi leo haiwezekani wawe na
nidhamu kwenye kile kipande cha kukaribia mita 200, 300 kwahiyo ule
utaratibu wa mtu kwenye gari kutupa taka hovyo mshusheni akikataa
chukueni namba yake ya gari tutamkamata ili aje apige deki” Amesema
Makonda.
Pia
amesema ifikapo Agosti 5 Jiji la Dar Es salaam liwe safi kwa ajili ya
mapokezi ya wageni na amewataka Maafisa Mazingira kuhakikisha miti yote
inayopandwa inaota kwani Serikali imekuwa ikitenga bajeti kubwa na pesa
hizo hazioneshi matunda na Mazingira chanya kama inavyokusudiwa.
Makonda
amewataka Vijana wa usafishaji kuhakikisha kwamba Dereva wa gari
akitupa taka taka hovyo apigishwe deki kwa kupewa kipande cha bara bara
badala ya kuwapiga faini za pesa na watendaji wa mitaa husika
kuhakikisha maeneo yao yanakuwa safi la sivyo watapoteza ajira zao.
Katika
hatua nyingine amewataka Wananchi na Tanzania kwa ujumla wajitokeze kwa
wingi katika uzinduzi wa Uwanja mpya wa ndege wa Kisasa wa Mwalimu
Nyerere Terminal 3 wenye uwezo wa kubeba Abiria Milioni 6 utakaotarajiwa
kuzinduliwa na Rais Dkt John Magufuli Agosti 4/2019 asubuhi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...