Na Charles James, Michuzi TV

Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) imesema mfumuko wa bei wa Taifa Kwa mwaka ulioishia mwezi jana umeongezeka hadi asilimia 3.7 kutoka asilimia 3.5 kwa mwaka ulioishia mwezi Mei, 2019.

Akizungumza na wandishi wa habari leo Jijini Dodoma, Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi, Daniel Masolwa ongezeko hilo linamaanisha kuwa kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioisha mwezi Juni imeongezeka ikilinganishwa na Kazi ya mwezi Mei.

" Ongezeko la mfumuko wa bei Kwa mwaka ulioisha mwezi Juni kumechangiwa na kuongezeka kwa bei za bidhaa za vyakula na bidhaa zisizo za vyakula kwa kipindi cha mwakamwaka ulioisha mwezi Juni, 2019 ikilinganishwa na Juni 2018.

" Baadhi ya bidhaa za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa mfumuko huo ni unga wa mahindi asilimia 3.6, ngano asilimia 4.4, mtama asilimia 4.9, samaki wabichi asilimia 27.3," amesema Masolwa.

Amesema bidhaa bidhaa zisizo za vyakula zilizochangia ongezeko hilo ni pamoja na dizeli kwa asilimia 11.4, payroli asilimia 4.9, nyumba za kulala wageni asilimia 5.8 na vitabu vya shule vikiwa ni asilimia 2.4.

Pia amefafanua hali ya mfumuko wa bei Kwa Nchi za Afrika Mashariki ambapo Uganda mfumuko wa bei ulioishia Juni mwaka huu ulikua asilimia 3.4 kutoka asilimia 3.3 huku Kenya ongezeko likifikia asilimia 5.70 kutoka asilimia 5.49.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...