Na Said Mwishehe,Michuzi TV

SHIRIKA la Umeme Tanzania( TANESCO) wameibuka washindi wa pili katika Category ya Nishati na Madini katika Maonesho ya Biashara ya 43 ya Kimataifa yanayoendelea viwanja vya Mwalimu Nyerere, Sabasaba jijini Dar es Salaam.

TANESCO wametangazwa kuibuka na ushindi wa nafasi hiyo ya pili leo baada ya Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan kuzindua rasmi maonesho hayo yaliyoanza Juni 28,mwaka huuu wa 2019.

Nafasi ya kwanza imechukuliwa na Tume ya Madini na kwamba walioshinda tuzo hizo ni baada ya majaji zaidi ya 25 kuchuja washiriki kwa video ambavyo vimewekwa katika kupata washindi ambapo tulikuwa na Category 27.

Baadhi ya vigezo ambavyo vimetumika kupata washindi kwa makundi mbalimbali ni ubora wa bidhaa, upambaji wa mabanda, namna wanavyohudumia wateja pamoja na namna washiriki anavyoweza kuielezea kauli mbiu ya mwaka huu inayosema Usindikaji wa Mazao ya Kilimo kwa maendeleo ya viwanda.

Hata hivyo tangu kuanza kwa maonesho hayo Juni 28,2019 TANESCO wamekuwa wakitoa huduma mbalimbali ikiwemo ya kusikiliza kero za wateja wao na kuzipatia ufumbuzi pamoja na kueleza kazi wanazofanya huku pia wakitumia maonesho hayo kuzuzungumzia miradi mikubwa ya umeme nchini ambayo utekelezaji wake upo hatua mbalimbali.

Akizungumzia tuzo ambayo wameipata wakati akiwa kwenye banda la shirika hilo katika maonesho ya biashara Sabasaba jijini Dar es Salaam, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Usambazaji wa Umeme na Huduma kwa Wateja TANESCO Mhandisi Raymond Seya amesema hiyo imetokana na maandalizi ambayo wameyafanya na kubwa zaidi ni kuwa karibu na wananchi katika kupatia huduma ya nishati ya umeme.

"Tuzo hii inatufanya TANESCO tuendelee kuwa karibu na wananchi na tutaendelea kuchapakazi kwa ajili ya Watanzania wote kwa kuhakikisha tunatekeleza mipango na mikakati ambayo tumeiweka kuhakikisha nchi inakuwa na nishati ya umeme wa kutosha na wa uhakika," amesema Mhandisi Seya.

Ameongeza kuwa TANESCO inaendelea kuboreka na changamoto chache zilizopo wanakabiliana nazo,kimsingi kuhakikisha nishati ya umeme nchini inapatikana ya kutosha huku akiwaomba wananchi kwa ujumla kuendelea kuchangamkia punguzo la gharama za kuunganishiwa umeme kutoka Sh.300,000 hadi kufikia Sh.27000 bila kujali mwananchi aliwepo awe mjini au kujijini.

Pamoja na mambo mengine Mhandisi Seya amesema TANESCO wanajivunia kuongeza idadi ya wateja wanaowahudumia na ongezeko hilo limetokana na mradi wa kuunganisha umeme vijijini kupitia Wakala wa Umeme Vijijini(REA) pamoja na kuwaunganishia umeme wateja wakubwa wanaomiliki viwanda vikubwa na vya kati.

Mhandisi Seya pia amegusia miradi mikubwa ya umeme nchini inayoendelea kutekelezwa ukiwemo mradi wa umeme Mto Rufiji ambapo amesema TANESCO wanahusika kwa asilimia kubwa kuusimamia na tuzo ambayo wameipata kwenye maonesho hayo inawapa hamasa kuendelea kujituma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...