Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
VIJIMAMBO bidhaa zetu zina ubora unaokidhi viwango?Ndivyo anavyoeleza Katibu wa Kikundi cha Vijimambo Grace Ndege wakati anazungumzia bidhaa zao kwenye Maonesho ya Biashara yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
Kikundi cha Vijimambo wamejikita zaidi kwenye bidhaa za kutengeneza dawa lishe kwa ajili ya kutibu maradhi mbalimbali kwenye mwili wa binadamu ikiwemo dawa inayotibu pumu, vidonda vya tumbo, gesi pamoja na dawa za kuzuia kukoroma wakati ukiwa umelala
Akifafanua zaidi kuhusu bidhaa zao kutokana na ubora wa bidhaa zao wananchi kutoka sehemu mbalimbali wamekuwa wakifika kwenye ofisiza kupata huduma kwa kununua dawa tiba ambazo zinatokana na mchanganyiko wa mazao.
"Dawa lishe ambazo tunatengeneza zimekuwa zikitibu magonjwa mbalimbali .tunazo dawa lishe za kuondoa gesi mwilini,kilungurila,vidonda vya tumbo na hata za kuondoa sumu mwilini. Pia tunazo dawa lishe za kuondoa aina mbalimbali ya fangasi mwilini, homa ya tumbo pamoja na inayotibu kuongeza uteute kwenye jointi kwa wale ambao wana matatizo ya kukosa uteute na hasa kwenye magoti kiasi cha kusababisha maumivu,"amesema Grasce Ndege.
Amesema kimsingi wanajiamini na bidhaa ambazo wanazitengeneza wao na katika kuhakikisha wanatengeneza dawa lishe zilizo na viwango wamefuata taratibu zote na wamekubalika na mamlaka zote za Serikali huku akitumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi wanaofika kwenye Maonesho ya Sabasaba kufika kwenye bandao lao kupata dawa lishe kwa gharama nafuu.
"Dawa zetu zina ubora wa hali ya juu, na sisi tumejikita zaidi na dawa lishe.Kwa sasa tupo Sabasaba na baada ya hapo tutapatikana kwenye ofisi zetu zilizopo Dar free Makert ,Machinga Komplex na Kigogo Kati,"amesema Grace Ndege.
Amefafanua kwa sasa dawa lishe inayofanya vizuri kwenye soko ni ya Brain Actvater ambayo ina mchanganyiko wa mbegu za matunda na nafaka zilizo hai.Pia wanayo dawa lishe kwa ajili ya watu wenye kusumbuliwa na areji.
Ametuimia nafasi hiyo kutoa ushauri kwa Serikali kuendelea kutoa elimu kwa wajasiriamaliili kuhakikisha wanadhalisha bidhaa zenye ubora unaokubalika na kutambua nakuwatangaza kokote wanakokwenda.
Pia ameiomba Serikali kuendelea kuwaunga mkono kwani wao ni wajasiriamali waliojikita
kwenye usindikaji na kikundi chao kinawatu watano lakini nyuma yao kuna kundi kubwa la Watanzania ambao wanahitahi bidhaa zao na kwamba wao wanaimani kubwa na Serikali ya Awamu ya Tano.
Grace Ndege akifafanua jambo kuhusu bidhaa wanazotengeneza na kikundi chao cha Vijimambo
Grace Ndege ambaye tupo kwenye kikundi cha Vijimambo wanaozalisha dawa lishe akiwa wateja ili wafike kwenye banda lake lililopo katika maonesho biashara ya Sabasaba jijini Dar es Salaam
Mmoja ya wananchi kuangalia bidhaa za dawa lishe zinazotengenezwa na Kikundi cha Vijimambo baada ya kutembelea banda la kikundi hicho lililopo katika Maonesho ya Biashara Sabasaba jijini Dar es Salaam





Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...