Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli (kulia) na Rais wa Zimbabwe Mhe. Komredi Emmerson Mnangagwa
Tanzania na Zimbabwe zimetiliana saini hati tano za makubaliano ya ushirikiano katika nyanja mbalimbali ikiwa ni kutekeleza maelekezo ya Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na Rais wa Zimbabwe Mhe. Komredi Emmerson Mnangagwa ya kuhakikisha nchi hizo zinashirikiana katika masuala ya kiuchumi ili kuleta maendeleo kwa wananchi wa nchi hizo.
Hati hizo za makubaliano zimesainiwa Harare Nchini Zimbabwe na Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi kwa upande wa Tanzania na Waziri wa Mambo ya Nje na biashara ya kimataifa wa Zimbabwe Luten Jenerali Mstaafu Sibusiso Moyo.
Akizungumza mara baada ya kusaini hati hizo za makubaliano waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. palamagamba Kabudi amesema mkutano huo unafanyika kwa mara ya kwanza baada ya miaka 21 na kuongeza kuwa uhusiano baina ya Tanzania na Zimbabwe ulianza kabla ya ukoloni na kuimarika zaidi wakati wa kupigania ukombozi na sasa ni wakati muafaka kwa nchi hizo kuanza mapambano mapya ya kiuchumi.
Makubaliano hayo yamefikiwa katika nyanja za ushirikiano wa biashara,uchumi na uwekezaji, siasa na diplomasia,utalii,uwezeshaji wa wanawake na masuala ya jinsia pamoja na masuala ya ujasiriamali mdogo na wa kati.
Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje na biashara ya Kimataifa Luten Jenerali Mstaafu Sibusiso Moyo ameshukuru kwa mkutano huo kufanyika baada ya kupita miaka mingi na kusisitiza kuwa jukumu lililosalia ni kuhakikisha utekelezaji wa makubaliano yaliyofikiwa yanafnyika kwa kasi kubwa ili kuleta maendeleo kwa wananchi wan chi hizo mbili.
Ametaka ushirikiano baina ya nchi hizo hususani katika nyanja ya uchumi usiachwe ukadorora kwa muda mrefu kama ilivyotokea katika kipindi kilichopita kwani kwa sasa maendeleo ni biashara na ushirikiano baina ya nchi na nchi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...