
Pichani
kulia ni Naibu Katibu Mkuu (EAC),Christopher Bazivamo akizungumza
kwenye Warsha ya siku moja mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani)
hivi karibuni kuhusu mradi
wa 50 Milioni African Women Speak
Networking,unaotarajiwa kuratibiwa nchini Tanzania ili kuwaunganisha
wanawake Wajasiriamali katika nchi za Jumuiya ya Afrika
Mashariki,Kushoto ni
Mkurugenzi wa Idara ya Jamii (EAC),Mary Makoffu.Picha na Michuzi JR.
Mkurugenzi wa Idara ya Jamii (EAC),Mary Makoffu.Picha na Michuzi JR.
Warsha hiyo ya Wanahabari ikendelea
Naibu
Katibu Mkuu (EAC),Christopher Bazivamo akifafanua zaidi kwenye Warsha ya
siku moja mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani) hivi karibuni
kuhusu mradi
wa 50 Milioni African Women Speak
Networking,unaotarajiwa kuratibiwa nchini Tanzania ili kuwaunganisha
wanawake ,pia katika nchi
za Ecowas na Commesa na lengo lake kubwa ni kuwawezesha wanawake
kiuchumi na hususani wanawake wajasiriamali,Pichani kulia ni Mkurugenzi wa Fedha (EAC) Juvenari Ndimurirwo na kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Jamii (EAC),Mary Makoffu
Mkurugenzi wa Idara ya Jamii (EAC),Mary
Makoffu(katikati) akizungumza mbele ya Waandishi wa habari (hawapo
pichani),kwenye Warsha hiyo ya siku moja iliofanyika jijini Dar,kushoto
ni Ofisa Maendeleo Mwandamizi
wa Wizara hiyo kutoka Idara ya Jinsia Mapunda John


Mkurugenzi wa Fedha (EAC) Juvenari Ndimurirwo akifafanua namna ya umuhimu wa kupanga na matumizi ya fedha katika mambo mbalimbali ikiwemo mradi wa Mradi wa 50 Milioni African Women Speak Networking,hasa kwa watakaosiriki kwa namna moja ama nyingine.
Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii.
WIZARA
ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto imeeleza faida za
upatikanaji wa taarifa muhimu zikiwemo za fedha kwa Wanawake
wajasriamali kwa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki na nchi nyingine
Barani Afrika.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Ofisa Maendeleo Mwandamizi
wa Wizara hiyo kutoka Idara ya Jinsia Mapunda John amesema wajasiriamali
hao wanaunganishwa kupitia mradi wa 50 Milioni African Women Speak
Networking.
Amesema ni
mradi ambao unatekelezwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki,pia katika nchi
za Ecowas na Commesa na lengo lake kubwa ni kuwawezesha wanawake
kiuchumi na hususani wanawake wajasiriamali.
"Kwa
Jumuiya ya Afrika Mashariki mradi unatekelezwa kwenye nchi sita. Na sio
jumuiya ya Afrika Mashariki tu bali hata katika nchi nyingine nje.
Kuhusu kuwawezesha wanawake kiuchumi ni katika suala zima la kuwapatia
taarifa muhimu ikiwa pamoja na taarifa za fedha na taarifa ambazo sio za
fedha.
"Sasa kwa maana
ya taarifa za fedha tunamaanisha taarifa kwa mfano za wapi mikopo
inapatikana ,wapi grants zinapatikana lakini ili waweze kutumia kama
mitaji kuendesha biashara zao lakini tunavyosema taarifa ambazo sio za
fedha kuna taarifa mbalimbali ambazo ni muhimu kwa wajasiriamali
kuzipata," amesema John.
Pia
amesema taarifa zinazohusu masoko na mambo mengine ya kutambua thaman
na wapi kwenye uhitaji na hata usalama wa biashara kwani kuna baadhi ya
nchi nyakati za uchaguzi hahuko salama ,hivyo lazima wajasiriamali hao
wawe na taarifa.
Amesisitiza
kwamba lengo kubwa la mradi huo ni kuhakikisha ni namna gani taarifa
hizo zitawafikia wanawake wajasiriamali na ndio maana matarajio ni
kuandaliwa kwa Website ambayo ndani yake kutakuwa kunawekwa taarifa zote
muhimu.
"Na kwamba si tu
bali wanafikiria kwa kuwa na eneo moja la wajasiriamali kukutana
watakuwa na mijadala mbalimbali kati ya wafanyabiashara wakubwa na
wakati ikiwa pamoja na kubadilishana uzoefu," amesema John.
Amefafanua
kuwa wameona kuwa wanaweza kutengeneza Website nzuri na kuwekwa taarifa
zote lakini kama wanawake wajasiriamali hawajui haitakuwa na maana
yoyote.
Hivyo amesemani
fursa muhimu kwao kukutana na vyombo vya habari kwani kwa kutumia njia
zao za kufikisha taarifa watawafikishia wanawake wajasiriamali taarifa
za nchiradi huo na wanafanya hivyo kwa kuamini kuna takribani ya
wanawake milioni 500 na malengo ni kuwafikia wanawake asilimia 10 ambayo
ukiiigiwa unapata wajasiriamali milioni 50 kwa jumuiya tatu ambazo kuna
nchi 38.
"Wanawake wapo
wengi,wapo ambao wamefanikiwa na wapo ambao hawajafanikiwa.Kwa kutumia
Poto hii au Website tunaamini itakuww chachu ya maendeleo yao na nchi
husika kwa ujumla," amesema John.









Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...