Tume
ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC), inatarajia kushiriki kwenye
maadhimisho ya sherehe za kitaifa za Nane Nane kanda ya ziwa mashariki
yatakayofanyika katika viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu kuanzia
tarehe 28 Julai hadi 10 mwezi Agosti, 2019.
Katika
maadhimisho hayo, TAEC itaweza kuonesha shughuli mbali mbali
zinazofanyika katika Tume ikiwemo utoaji wa elimu kwa wananchi na wadau
mbali mbali juu ya udhibiti na matumizi salama ya mionzi hapa nchini.
Elimu
kwa wananchi kuhusu matumizi salama ya teknolojia ya nyuklia kwenye
sekta za afya, kilimo, viwanda, mifugo, maji, lishe pamoja na ujenzi
inatolewa.
Wananchi
wote wanakaribishwa ili kuweza kujipatia elimu bure kwa njia za
maelezo, video fupi, vipeperushi na majarida ili kujiongezea uelewa juu
ya majukumu yanayotekelezwa kisheria na TAEC katika Nyanja za udhibiti
wa mionzi na uhamasishaji wa matumizi salama ya teknolojia ya nyuklia.
Imetolewa na ,
Peter Ngamilo
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano
Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...