Benki ya NBC imeahaidi kuendelea kutoa huduma bora zenye ubunifu kwa Mamlaka za serikali ya mtaa hapa nchini ili kuongeza tija na ufanisi zaidi kwa mamlaka hizo.

Ahadi hiyo imetolewa na Meneja Mahusiano ya Kiserikali wa NBC, Bw William Kallaghe wakati akizungumza kwenye kwenye Mkutano wa Mkutano Mkuu wa 35 wa Mwaka wa Jumuiya za Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) uliofanyika hivi karibuni jijini Mwanza hivi karibuni.

Alisema katika kipindi cha miaka 50 ya uwepo wa benki hiyo hapa nchini, imewekeza katika huduma mbalimbali za kifedha ambazo zimeleta tija kubwa kwa mamlaka hizo na taifa kwa ujumla.

“Katika kipindi chote hicho NBC tumefanikiwa kutoa suluhisho ya kiubunifu kupitia huduma za kielectroniki kwa Halmashauri za Wilaya na Manispaa katika ukusanyaji wa mapato sambamba na huduma za malipo zinazoboresha usahihi katika uendeshaji akaunti’’ alisema.

Alibainisha kuwa uwezo huo umeimarishwa zaidi kufuata mfumo wa Malipo ya Serikali Kielektroniki (GePG),Mtandao wa NBC Wakala, Mfumo wa makusanyo wa POS pamoja na makusanyo kupitia simu za mikononi.

Kwa mujibu wa Bw Kallaghe, huduma za kielektroniki za malipo na ukusanyaji wa mapato zinazotolewa na benki ya NBC kwa mamlaka hizo zimeongeza ufanisi katika malipo na ukusanyaji wa mapato kwa mamlaka hizo na hivyo kurahisisha usahihi katika uendeshaji wa akaunti zao.

“Matawi ya NBC yamewezeshwa kwa nyanja zote katika kufanikisha mahitaji yote ya kifedha kwa Halmashauri na Mamlaka zote za serikali ya mitaa,’’ alibainisha huku akiongeza kuwa lengo kuu ni kuhakikisha mamlaka hizo zinatoa huduma bora na za kisasa sambamba na kujiongezea mapato.


Mkuu wa Kitengo cha Kibenki cha Taasisi za Sekta ya Umma kutoka Benki ya NBC, Bi. Noelina Kivaria akipokea cheti cha utambuzi kutoka kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa ikiwa ni utambuzi wa mchango wa benki hiyo katika kufanikisha Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Jumuiya za Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) uliofanyika hivi karibuni jijini Mwanza. Anaeshudia ni Mwenyekiti wa Alat Taifa, Gulamhafeez Mukadam (kushoto). Benki hiyo ilikuwa ni moja ya wadhamini wa mkutano huo.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa akipata maelezo ya huduma za kibenki kutoka kwa Meneja Mahusiano ya Kiserikali wa NBC, Bw William Kallaghe alipotembelea kwenye banda la benki hiyo kwenye Mkutano wa Mkutano Mkuu wa 35 wa Mwaka wa Jumuiya za Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) uliofanyika hivi karibuni jijini Mwanza. Wengine ni Mkuu wa Kitengo cha Kibenki cha Taasisi za Sekta ya Umma, Bi. Noelina Kivaria. Benki hiyo ilikuwa ni moja ya wadhamini wa mkutano huo.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa akisoma moja ya machapisho ya huduma za kibenki ya Benki ya NBC alipotembelea kwenye banda la benki hiyo kwenye Mkutano wa Mkuu wa 35 wa Mwaka wa Jumuiya za Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) uliofanyika hivi karibuni jijini Mwanza. Kushoto ni Meneja Mahusiano ya Kiserikali wa Benki ya NBC, Bw William Kallaghe pamoja na maofisa wengine wa benki hiyo. Benki hiyo ilikuwa ni moja ya wadhamini wa mkutano huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...