Na Said Mwishehe,Michuzi TV

TAASISI inayowakilisha elimu ya Vyuo Vikuu vya Nje nchini Tanzania(UAR) imesema kwa sasa muitikio wa Watanzania kwenda kusoma nje ni mkubwa.

Pia ismesema wanafarajika kuwepo kwenye Maonesho ya Biashara ya 43 ya Kimataifa yanayoendelea Sabasaba jijini Dar es salaam kwani ni fursa kwao kutumia wingi wa watu wanaofika kwenye maonesho hayo kuzungumza nao.

Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya UAR nchini Tanzania Tony Kabetha amesema hayo kwenye Maonesho ya Biashara yanayoendelea jijini Dar es Salaam ambapo nao wameweka banda kueleza shughuli wanazofanya.

“Sisi kama taasisi tunathamini nakutambua mkusanyiko wa watu kwasababu kubwa mbili, kwanza sisi ni washauri kwa watanzania nini cha kusoma ukizingatia suala la ajira na tunatambua Vyuo vikuu vingi vinafundisha elimu ya jumla(General Education).

“Kwa hiyo tumekuja na ufadhili wa masomo kutoka nje ya nchi lakini hatujakubali Scolashirp zote bali tumechagua zile ambazo zinaendana na mahitaji ya nchi kwa sasa kulingana na sera za nchi,”amesema Kabetha

Pia amesema wanatoa ushauri kwa Watanzania wakasome nini kuhusiana na hiyo sera ambayo itawapa ajira na itawatayarisha kwenye akili zao kwenda kujitegemea wao wenyewe.

“Kwa hiyo nafurahi kusema Serikali ya India na Serikali ya China wametoa hizo Scola shirp zaidi ya 200 ambazo Watanzania watakwenda kusoma kwa gharama nafuu na ndogo sana na wengine watakwenda kusoma bure.

“Pia wengine watakwenda kusoma kwenye vyuo vikuu ambazo gharama zake ni sawa na vyuo vya Tanzania.Na masomo ambayo yamechaguliwa ni mambo ya teknolojia ya viwandani, mambo ya utengenezaji dawa , usindikaji na masomo yanayohusu biashara pamoja na aina nyingine ya masomo kulingana na mahitaji ya mhusika”amesema.

Ameongeza pia masomo ya teknolojia ya kompyuta huku akifafanua hawajasahau masomo yanayohusu elimu ya tiba ya afya.Pia tumechukua wanafunzi wote wa masomo ya Art ili kwenda kusoma masomo mbalimbali,”amesema.

Hivyo amesema taasisi ya UAR inawakaribisha vijana wote waliomaliza ngazi ya Diploma, Digrii na Mastars.Pia wale waliomaliza elimu ya kdato cha sita ambao wanajiandaa kwenda vyuo vikuu.

Akizungumzia muitikio wa Watanzania kwenda kusoma nje , amesema kwa sasa kwa sasa muitikio ni mkubwa kwani kila mmoja anataka kwenda kusoma nje na kuna maelfu ya Watu ya wanataka kwenda na changamoto inakuwa uwezo wa wazazi kwani wengine hawana hata nauli.

Hata hivyo amesema kutokana na muamko wa vijana wa Tanzania kwenda kusoma nje ya nchi kupitia taasisi yao kuna wazazi wamekuwa wakilipa kidogo kidogo na kufafanua changamoto iliyopo nafasi ni chache kuliko idadi ya wanaohitaji.

“Baada ya Maonesho ya Sabasaba tunapatikana pale Posta Mpya katika jengo la Mkapa jijini Dar es Salaam.Ukifika kwenye jengo hilo nenda ghorofa ya kwanza na uliza UAR , basi utafikishwa tulipo. Pia tupo mikoani ambako nako tuna ofisi zetu,”amesema Kabetha.
 Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya UAR nchini Tanzania Tony Kabetha pichani kulia alipokuwa akizungumza na Michuzi TV,leo kwenye banda lake ndani ya  Maonesho ya Biashara almaarufu saba saba yanayoendelea jijini Dar es Salaam, ambapo alieleza shughuli wanazofanya.

“Sisi kama taasisi tunathamini nakutambua mkusanyiko wa watu kwasababu kubwa mbili, kwanza sisi ni washauri kwa watanzania nini cha kusoma ukizingatia suala la ajira na tunatambua Vyuo vikuu vingi vinafundisha elimu ya jumla(General Education).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...