Mjumbe wa Halmashauri kuu Taifa Japhary Kubecha akikata utepe kuashiria Uzinduzi wa shina la Chama cha hicho wetulopo eneo la Mwembe radu, Mwembe Yanga Wilayani Temeke.
Mjumbe wa Halmashauri kuu Taifa Japhary Kubecha akisoma jumbe zilizoandikwa kwenye shina hilo la Mwembe radu,Wilayani Temeke.
Mjumbe wa Halmashauri kuu Japhary Kubecha akizungumza mbele ya wanaCCM waliojitokeza katika Uzinduzi wa shina la Mamboleo Lililopo Sandari,Wilayani Temeke.
Mjumbe wa Halmashauri kuu Taifa Japhary Kubecha akivishwa kitambaa shingoni na vijana chipukizi wa Chama hicho wakati akizindua shina lililopo ndani ya Kata ya Sandari Wilayani Temeke leo .picha na Mpiga picha wetu.
Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo mkoa wa Dar Es Salaam Mussa Kilakala kushoto akiwa sambamba na Mjumbe wa Halmashauri kuu Taifa Japhary aliyevaa kofia meza kuu pamoja na viongozi wengine wa Jumuiya hiyo Kata na Matawi..
Burudani
Katibu wa Kata ya Sandari wa Jumuiya ya Vijana Mrisho Kamba akizungumza mbele ya wanaCCM katika mkutano uliofanyika katika Ofisi za Kata hiyo ya Sandari Wilayani Temeke.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana Kata Sandari kushoto akiwa pamoja na Mjumbe wa Halmashauri kuu Japhary Kubecha wakisubiri kuzungumza na waandishi wa Habari moja ya ofisi za Chama Kata ya Sandari Temeke Dar Es Salaam.
MJUMBE wa Halmashauri kuu Taifa kupitia Jumuiya ya Umoja wa Vijana UVCCM Jafaphary Kubecha amewataka wanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM kuhamasika na kuendelea kuunga mkono kazi kubwa inayofanywa na Rais Dkt.John Magufuli ya kuijenga Tanzania.
Amesema tangu amechaguliwa kuwa Mjumbe wa Halmashauri kuu mapema mwaka huu kupitia Jumuiya ya vijana amefanya ziara katika mikoa kadhaa na Wilaya zake ameshuhudia wanaCCM wakiwa na hamasa kubwa .
Kubecha ameyasema hayo Jijini Dar Es Salaam leo akiwa katika kazi maalum ya kufungua mashina ya Chama hicho yaliyopo ndani ya Kata ya Sandari Wilayani Temeke.
"Nawahamasisha wanaccm popote walipo kuendelea kuunga mkono kazi kubwa zinazofanywa na Rais Dkt Magufuli Mimi tangu nimechaguliwa katika nafasi hii nimeshafanya ziara mikoani na kwakweli wananchi na wanaCCM wanahamsika sana ." amesema Kubecha
Pia katika hatua nyingine amewataka wanachama wa Chama cha Mapinduzi kujiandaa na uchaguzi wa Serikali za mitaa ambao unatarajia kufanyika mwaka huu na uchaguzi Mkuu ujao mwaka 2020.
Akizungumza wakati akizindua mashina hayo amewataka wanachama wa Chama chake kuenzi matawi hayo na kamwe wasigeuze kuwa sehemu ya vijiwe vya kukutania.
"Nawaomba mashina haya yawe chachu ya kujenga umoja miongoni mwenu na kufanya kazi za kuimarisha chama chetu na msitumie matawi haya kama sehemu ya kupigia stori na vijiwe vya kufanya mambo yasio stahili.
Pia akizungumzia changamoto iliyojiyokeza ndani ya chama juu ya walaka ulioandikwa na wazee wa Chama hicho ambao pia wamewahi kuwa viongozi wakuu watendaji amesema walaka huo hauna mashiko.
Amesema wazee hao wanajua utaratibu wa Chama na si kuandika walaka ambao mwisho wasiku wanaposti kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii jambo ambalo si sahihi.
" Chama hiki kina utaratibu wake na kwa bahati nzuri wote tunajua hivyo walaka huo kwasababu haujapita kwenye utaratibu wa kichama upita kwenye mitandao basi hatuwezi kufanyia kazi jambo ambalo limepitishwa huko."amesema Kubecha.
Naye Katibu wa Jumuiya ya Vijana Kata ya Sandari Mrisho Kamba amewataka Vijana wa chama cha Mapinduzi CCM kujipanga vema kuelekea uchaguzi wa Serikali ya Mtaa na huku wakiendelea kuyazungumzia mazuri yanayofanywa na Mwenyekiti wao wa Chama Taifa na Rais Dkt John Magufuli.
Pia amewataka Jeshi la Polisi kutoa kibari kwa vijana hao wa Chama kushughulika na watu ambao wanasema maneno ya hovyo dhidi ya Rais Dkt. Magufuli.
"Ndugu mjumbe wa Halmashauri kuu Taifa Ndugu Kubecha tunaomba tufikishie salamu kwa mh Rais wetu .kwamba tupo tayari kuwashughulikia watu ambao hawaoni kazi anayofanya katika nchi hii na kwamba Polisi wawaache wawafunze adabu." Amesema Kamba
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...