Na Said Mwishehe,Michuzi Blog

WADAU wa mazingira nchini na hasa wanaokabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchini wameiomba kuhakikisha wagunduzi na wabunifu wa nishati jadidifu wanapewa kipaumbele na kusaidiwa.

Wakati kwa upende wa Serikali umesema ugunduzi na ubunifu katika nishati jadidifu ihusishayo nishati endelevu ni miongoni mwa fursa inayoleta ajira,kuongeza uzalishaji,ubunifu na kupunguza umasikini katika kuiletea nchi maendeleo endelevu na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Pia imesema jamii inapaswa kubadili mtazamo na kufungua upeo zaidi kwa kuyaona masuala ya nishati jadidifu kwa jicho chanya kwa kuwa yanatoa fursa mbalimbali za kibiashara na uzalishaji.

Akizungumza wakati wa Jukwaa la Mabadiliko ya Tabianchi kwenye Maonesho ya biashara Sabasaba, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara ( TANTRADE)Ratifa Hamisi kwa niaba ya Waziri wa Nchi,Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingira January Makamba amesema Serikali inatambua uwepo wa wabunifu wa kada mbalimbali katika kanuni nishati jadidifu kama moja ya mkakati wa kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Akifafanua zaidi kwenye Jukwaa la Mabadiliko ya Tabianchi ambalo limeandaliwa na Shirika la FORUMCC chini ya mradi wa kutoa elimu kuhusu nishati Jadidifu kupitia ufadhili wa taasisi inayoshugulikia masuala ya Nishati Jadilifu inayofahamika kwa jina la Hivos amesema Serikali inatambua changamoto zitokanazo na uharibifu wa mazingira na athari za mabadiliko ya tabianchi kufikia katika maendeleo ya uchumi wa kati .

Amesema utumiaji wa nishati jadidifu utasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza athari hizo za mabadiliko ya tabia nchi. "Changamoto hizo zimeathiri uzalishaji katika sekta ya kilimo ambayo ndio inachangia kwa kiasi kikubwa malighafi za viwanda,uhaba wa maji ambayo hutumika viwandani na uzalishaji wa nishati na uharibifu wa miundombinu ambayo hutumika kukutanisha malighafi, viwanda na masoko,tunaamini utumiaji wa nishati yadilifu itasaidia Kwa kiasi kikubwa kuondokana na janga hili la mabadiliko ya tabianchi," alisema

Ameongeza kutokana na jitihada za Serikali ikishirikiana na washirika wa maendeleo, sekta binafsi na asasi za kiraia, matokeo chanya ya lengo hilo yanaonekana kwani takwimu za sasa zinaonesha takribani nyumba milioni 26 (sawa na watu milioni 100) wanatumia nishati jadidifu .

Amesema nishati jadidifu katika Tanzania inahitaji mpango wenye taarifa sahihi za sekta ya nishati jadidifu ili kuweza kuainisha njia za maendeleo za baadae na kuhakikisha watunga sera na wafanya maamuzi wana taarifa sahihi kuhusu nishati mbadala. 

"Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Nishati na Madini imetoa mpango wa mfumo wa umeme tangu mwaka 2016 (The 2016 Power System Master Plan (PSMP))mfumo huu unazingatia ukuaji wa uchumi na sera za serikali na miongozo.

"Ambapo miongozo ya sera ni pamoja na utayari wa Serikali kukuza uchumi kupitia dira ya 2025, MKUKUTA na Mpango wa Miaka Mitano (Five-Year Development PlanII (2016/17-2020/21, FYDPII)ambapo moja ya matokeo ya mpango huu ni kukuza uchumi kwa asilimia 10 ifikapo mwaka 2021 na kupunguza umaskini kwa asilimia 16.7 kutoka asilimia 28.2 ya mwaka 2011/12," amesema

Kwa Upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Wakala wa Nishati Vijijini(REA) Mhandisi Amos Maganga ameeleza wao wanatambua na kuthamini mchango unaotolewa na wabunifu wa vyuoni na wabunifu binafsi katika kuzingatia maendeleo ya nchi.

"Takribani miradi 20 REA imeweza kuwasaidia wabunifu mbalimbali katika kuhakikisha wanafanya kazi zao za kiubunifu ipasavyo na kusaidia nchi katika kuondokana nachangamoto mbalimbali.

''REA kuna programu ambazo zinaendelea na tumekuwa tunawasaidia wabunifu mbalimbali Kutoka vyuoni au wale wabunifu binafsi kwani tuna takribani fedha kupitia kwa wahisani dolla Milioni 19 sawa na zaidi ya Bilioni 40 ambazo zipo Kwaajili ya wabunifu Na wanaoweka miradi ya nishati bora vijijini,"amesema Mhandisi Maganga

Wakati huo huo Mkurugenzi wa Shirika la ForumCC Rebecca Muna amezungumzia umuhimu kwa Tanzania ya viwanda kuwa na nishati ya uhakika lakini ni vema kuangalia kuna fursa gani kama nchi ambazo zitatumika kuleta maendeleo huku kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Hata hivyo Muna ametoa mwito kwa wabunifu kuona fursa iliyopo katika nishati jadilifu huku kwa Serikali akiishauri kuanza kutengeneza mazingira mazuri kwa sera na sheria katika kulea na kukuza vipaji vya wabunifu katika sekta hii ya nishati jadidifu .Amesisitiza kwamba "Kama vipaji hivi vikiendelezwa kwa wabunifu wetu tutaweza kuchangiza kwa kiasi kikubwa sana upatikanaji wa nishati safi na salama kwa viwanda vyetu nchini."

"Tanzania tunavyanzo vya asili vingi sana hivyo uwekezaji ukifanya katika vyanzo hivyo tunauwezo mkubwa wa kuzalisha nishati jadidifu ikiwemo kinyesi cha mifugo," amesema Muna

Kwa upende wake Adam Nalima ambaye ni Mwanafunzi wa Chuo cha Mtakatifu Joseph,amesema wao waliamua kuja na wazo la kuhalikisha wanaboresha mazingira nchini ambalo lilikuwa ni uzalishaji wa umeme kwa njia ya nishati jadilifu kwa kutumia jua na upepo kwa wakati mmoja.
Hata hivyo wadau wa mazingira wakati wa majadiliano wanaonesha kutofurahishwa na kasi kubwa ya uharibifu wa mazingira ambayo athari zake imeanza kuonekan ikiwemo joto kupanda kiasi katika baadhi ya nchi akitolea mfano ya India watu waliopoteza maisha kwasababu ya joto kali.
 Baadhi ya wadau wa mazingira wakifuatilia masala wakati wa kongamano la Jukwaa la Mabadiliko ya tabianchi ambako limeandaliwa na FORUMCC
 Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara(TANTRADE) Ratifa Hamisi(katikati) akisikiliza maelezo ya mmoja ya wagunduzi wa nishati jadidifu kutoka Chuo Kikuu cha Nelson Mandella Profesa Njau (kushoto) wakati wa kongamano la Jukwaa la Mabadiliko ya tabianchi
Mdau wa mazingira na hasa katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ambaye anajihusisha  na utengenezaji wa mkaa mbadala Yusta Kibona akifafanua kuhusu nishati jadidifu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...