Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Mwenyekiti wa Bodi wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange amewaagiza wakandarasi wanaoendelea na ujenzi  wa Tenki la Kisarawe kukamilika kulingana na  makubaliano  ya mkataba.

Mradi huo unatekelezwa na DAWASA ikiwa ni katika jitihada za kuboresha huduma za maji kwenye enye ujazo wa Lita Milioni 6.

Mradi huo utahudumia maeneo ya Pugu, Gongo la Mboto, Airwing, Ukonga na Majohe unatarajia kukamilika kufikia Septemba mwaka huu.

“Mradi huo ambao ulianza rasmi mwaka jana unategemea kukamilika September mwaka huu utanufaisha wakazi wa KIsarawe, Pugu, Gongo la Mboto, Ukonga pamoja na Airwing kwa Upatikanaji wa  maji ya uhakika,”amesema

Ameeleza kuwa, mradi mpaka sasa umefikia pazuri na kutaka wakandarasi waongeze juhudi katika kukamilika kwake kulingana na makubaliano ya mkataba.

“Mpaka sasa Maendeleo ya Mradi ni mazuri na nina amini Mpaka kufikia Septemba mwaka huu wameniahidi  utakuwa umekamilika na Wanachi wa wilaya ya Kisarawe na vitongoji vyake watanufaika kwa kupata maji safi na salama,”alisema Mwamunyange.

Mbali na hilo, Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo  amemshukuru Rais John Pombe Magufuli pamoja  na DAWASA kwa kupeleka mradi wa maji Kisarawe utakaowezesha wananchi kupata huduma ya maji safi na salama pamoja na kuwezesha wawekezaji aa Viwanda kuwa na maji ya uhakika kwa ajili ya uzalishaji.

Dc Jokate amesema, Changamoto Sugu Ya Maji Mji Mdogo wa Kisarawe lenye Kata Nne Kuwa Historia Ifikapo September 2019 mwaka huu.

"Leo nimepokea ugeni ukiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya DAWASA Mkuu wa Majeshi Ya Ulinzi Tanzania- JWTZ Mstaafu Jen. Mstaafu Davis Mwamunyange, katika ziara ya kukagua maendeleo ya mradi ya maji utakaoleta maji, Mradi huu utanufaisha pia eneo letu maalum la Viwanda la Visegese lilopo eneo la kimkakati karibu na Reli mbili za TRC-SGR na TAZARA," amesema

Mradi wa Kisarawe unagharimu Bilion 10 na utahudumia wananchi wa Majohe, Pugu, Gongo la Mboto na maeneo ya Ukonga

Mwenyekiti wa Bodi ya DAWASA Mkuu wa majeshi mstaafu Jeneral Davis Mwamunyange alitembelea na kujionea Maendeleo ya ujenzi wa Tenki la kuhifadhia maji lenye ujazo wa Milioni sita pamoja na ujenzi wa tenki la Pugu  la ujazo wa lita milion 2.
 Mwenyekiti wa Bodi ya DAWASA Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali Davis Mwamunyange akitoa maelezo kwa Mkandarasi anayetekeleza ujenzi wa Tanki la maji la Kisarawe na kuwataka wamalize kwa muda kulingana na makubaliano ya Mkataba. Ujenzi huo ulianza July mwaka jana na unatarajiwa kukamilika mwezi Septemba mwaka huu.

 Mwenyekiti wa Bodi ya DAWASA Mkuu wa Majeshi mstaafu Jenerali Davis Mwamunyange wakiwa pampoja na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo baada ya kutembelea ulazaji wa mabomba yatakayosambaza maji katika kata zote za Kisarawe.
 Mwenyekiti wa Bodi ya DAWASA Mkuu wa Majeshi mstaafu Jenerali Davis Mwamunyange, Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo na watendaji wa DAWASA wakiwa kwenye picha ya pamoja  baada ya kutembelea ulazaji wa mabomba yatakayosambaza maji katika kata zote za Kisarawe.
Eneo la Pugu litakalojengwa tenki la maji lenye ujazo wa Lita Milioni 2 kwa siku.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...