WANANCHI wameshauliwa kujitokeza kwa wingi katika maonyesho ya sabasaba yanayoendelea jijini Dar Es Salaam ili kuweza kupata fursa ya kuona bidhaa mbalimbali ikiwa pamoja na kupata ushauri kuhusu afya na mambo mengine yanayohusu Binadamu.

Ushauri huo umetolewa leo na Mkurugenz wa huduma za kitabibu Aziza Bangoi Kutoka katika Kampuni ya Bangoi Natural Product ambaye naye nimiongoni mwa washiriki katika maonyesho hayo ya 43 ya kimataifa ya sabasaba ambapo yanafanyika kila mwaka mwezi kama huu.

Amesema ifike mahala Jamii ione umuhimu wa kuhudhuria kwa wingi kwenye maonyesho kama hayo kwani pamoja na mambo mengine lakini watapafursa ya kupata ushauri mbalimbali wa kiafya na hatimaye kuponya miiili yao ukizingatia miaka hii magonjwa yamekuwa mengi ukilinganisha na miaka mingi 

"Hapa kwenye maonyesho kuna vitu vingi wakiwamo matatibu tupo hapa waje wananchi wapate huduma kwa mfano Mimi hapa nina tiba za aina mbalimbali kama vile pumu,Ngili, virutubisho vya aina mbalimbali hivyo wafike hapa Banda la namba 32 la Ally Hassan Mwinyi watakutana na wataalumu wangu.amesema mama Bangoi.

Aziza amesema kuwa watanzania wanasumbuliwa na matatizo mbalimbali ya kiafya lakini tatizo kubwa ni watu ambao wanasubili hadi madhara wajitokeze waziwazi na ndio utaona wanahangaika kutafuta tiba badala ya kufanya hivyo mapema zaidi iwezekanavyo.

Amefafanua kuwa wa Serikali wameendelea kufanya vizuri katika kuenzi maonyesho hayo ambayo kimsingi dhamira kuu niwataka watanzania kupata wasaa kuja kuonyesha kile ambacho wanakifanya katika shughuli zao za kila siku na si vinginevyo hivyo niwajibu wa watanzania kujitokeza kwa wingi.

" ukifika katika Banda hili la Ally Hassan Mwinyi namba 32 utapata fursa ya kupata ushauri kwa magonjwa kama vile matatizo ya Meno,pumu,Mafuta ya nywele,ngozi ,dawa za nywele, fangasi,kupooza, ushauri wa namna ya kuacha pombe,na dawa zake zinapatikana hapa."amesisitiza Aziza

Pia katika eneo la vya kula lishe kama vile unga ya milonge,unga wa maboga,parachichi na pia anaondoa makemikali katika mwili wa binadamu hivyo wananchi wajitokeze kwa wingi katika viwanja hivyo vya sabasaba .

Aziza pia anatoa mwito kwa akina mama kuhamasika na kujitokeza kwa wingi kwani wao ndio wanamatatizo mengi na makubwa hivyo wasibaki makumbani watembelee viwanja vya maonyesho sabasaba.lakini hata msimu wa sabasaba ukimalizika wananchi wanaweza kufika maeneo ya Tandika nyumba na 47 Mtaa wa mwani Transfoma.
Mama Aziza Bangoi akiwa katika Banda lake namba 32 Banda la Ally Hassan Mwinyi akijaribu kutoa maelezo kwa mteja ambaye alifika katika Banda hilo ili kupata ushauri na tiba .kwenye viwanja hivyo vya maonyesho sabasaba .picha na Mpiga picha wetu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. A Vip free sms bomber which is working 100% for ios and android.
    We find satta king a india's best website to show satta results.

    ReplyDelete

  2. KL plumber offer fast, reliable & affordable plumbing services in Kuala Lumpur (KL), Petaling Jaya, Puchong, Damansara, Cheras, Shah Alam, Klang.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...