Na Woinde Shizza Michuzi Tv,Arusha
Kiwanda cha kutengeneza nguo na vyandarua cha A to Z,kilichopo mkoani hapa kimelipongeza shirika la kuhudumia viwanda vidogo hapa nchini mkoani Arusha(SIDO) kwa mradi wao wa kaizen ambao unafadhiliwa na shirika la maendeleo la watu wa japan(JIKA) kwa kuwawezesha kupata mbinu mbalimbali za kuendesha kiwanda chao hali iliyopelekea kushinda tuzo ya kimataifa.
Akizungumza Meneja wa uzalishaji wa kiwanda hicho Marko Ayo alisema kwamba tulikua na tatizo la ubora katika kiwanda chetu ambapo
alisema Kaizen imewasaidia kutatua tatizo hilo na kuwaongezea ujuzi zaidi hivyo kuongeza uzalishaji na ubora zaidi.
Kwa upande wake meneja wa ubora wa kiwanda hicho Dominick Marike alisema kwamba kwa sasa wataongeza mashine katika kiwanda hicho na
kwamba afya na ubora katika kiwanda hicho zitasimamiwa vizuri ikiwa ni kuhakikisha kuwa ubora wa wafanyakazi utazingatiwa vizuri.
Naye Ruben Lyanga,Afisa usimamizi wa ubora amesema kuwa zana za kaizen wamezipata na kwamba ni bora hasa katika maendeleo ya viwanda na kuongeza kuwa kwa kuwa kwa kutumia ujuzi wa kaizen ndio kulikofanikisha kunyakua tuzo hiyo.
“Kiwanda chetu kimenufaika sana na mafunzo ya kaizen mliyotupatia,tumeyatekeleza kwa vitendo na ndio sababu tumetoa tuzo hii na imetufanya kuongeza uzalishaji zaidi na kwa ubora
mkubwa”alisema Lyanga.
Kwa upande wake meneja wa shirika la kuhudumia viwanda vidogo nchini mkoa wa Arusha(SIDO) Linah Nchimbi alikishukuru kiwanda hicho kwa tuzo
hiyo waliyowapatia ambapo aliwataka wadau wengine wa viwanda vingine wafike SIDO kupata mafunzo ya kaizen.
“Nampongeza sana rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli kwa kuweka msisitizo juu ya uanzishaji wa viwanda vidogo na ndilo jukumu tunalolifanya sisi na tutahakikisha Tanzania ya viwanda inawezekana”alisema nchimbi.
Ameongeza kuwa wale wote wanaopata mafunzo hayo wanatakiwa waende katika maeneo ya uzalishaji na kuyafanyia kazi mafunzo hayo ili yawe
na tija na ufanisi zaidi.
“Tunahitaji wajasiriamali,wenye viwanda vidogo,vya kati wajitokeze zaidi ili kupata mafunzo ya kaizen kwani hadi sasa tuna wakufunzi zaidi ya 40 katoka wilaya zote za mkoa wetu wa Arusha”.
Meneja wa SIDO mkoa wa Arusha Linah Nchimbi akitoa mada kwa vijana kutoka majukwaa ya vijana wilaya ya Arusha waliotembelea makao makuu ya SIDO mkoa wa Arusha kujifunza mambo mbalimbali


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...