Na Woinde Shizza Michuzi Tv,Arusha.

WANAWAKE wameshauriwa kuendelea kuzingatia matumizi sahihi ya vipodozi vilivyoidhinishwa na mamlaka za kiserikali ili kuepukana na magonjwa hatari ya ngozi yanayotokana na matumizi ya vipodozi vyenye kemikali hatari kwa afya za watumiaji.

Ushauri huo umetolewa na Dk.Irene Shayo wakati wa uzinduzi wa bidhaa mpya ya Ecollagen inayotengenezwa na kampuni ya Oriflame ya nchini Sweden .Bidhaa hiyo ni vipodozi vilivyotengenezwa kwa viambata asilia kama mimea na matunda na havina kemikali za viwandani.

“Bado kuna kiwango cha juu cha matumizi ya vipodozi vyenye kemikali hatarishi kwa afya ngozi miongoni mwa wasishana, wanawake na hata vijana wa kiume wa Tanzania, hivyo juhudi kubwa zinahitajika kuwaelimisha madhara ya matumizi ya vipodozi hivyo hatarishi”alisema Dk.Shayo.

“Wengi wanatumia vipodozi hivi kutokana na upatikanaji na bei zake kuwa rahisi, lakini madhara yake ni makubwa sana na ni chanzo cha maradhi hatari kama kansa ya ngozi na kuharibika kwa ngozi ndani ya kipindi cha muda mfupi”aliongeza Daktari huyo.

Alisema tafiti mbalimbali zilizofanywa na Madaktari na Wataalamu wabobezi wa vipodozi na afya ya ngozi umethibitisha kuwa kemikali hizo hatari hundoa seli za ngozi zinazoitwa Melanin ambazo ndizo zinazomfanya binadamu kuwa na rangi nyeusi.

“Kemikali hizo huondoa seli za Melanin ambazo ndiyo zinazolinda ngozi dhidi ya mionzi ya jua na hata moshi wa viwandani kwahiyo inakuwa rahisi kwa mtumiaji kushambuliwa na maradhi kama kansa ya ngozi”aliongeza Dk.Shayo.

Madhara mengine kwa watumiaji kwa mujibu wa Daktari huyo kwa wanawake wanaotumia vipodozi vyenye kemikali (mkorogo) ni pamoja na uwezekano wa kuzaa mtoto mwenye mtindio wa ubongo,ugumba na maradhi ya figo.

Utafiti uliofanywa na Profesa Msaidizi Kelly Lewis wa Chuo Kikuu cha Georgia Atlanta cha nchini Marekani kitengo cha Sosholojia nchini Tanznia kati ya mwaka 2000 hadi 2012 unaonyesha kuwa asilimia 30 ya wanawake kati ya milioni 23 nchini ambayo ni sawa na wanawake milioni 6 wanatumia vipodozi vyenye kemikali hatari.

Kwa upande wake mmoja wa maaifisa masoko wa kampuni hiyo ya Oriflame Maribel Mwenda alisema kampuni hiyo imekuja na mfumo wa mauzo wa moja kwa moja (networking marketing) biashara ya mtandao kwa lengo la kuzuia watu wasiowaaminifu kunakili (fake) biadhaa zao na kuziingiza sokoni.

“Kupitia mfumo huu watumiaji au wateja wanapata fursa tatu, kupendeza,kupata faida na kupata ajira na kipato cha uhakika kutokana na faida inayopatikana katika mauzo”alisema.

Naye Suzan Mlay ambaye ni Mkurugenzi mwenye hadhi ya Juu (Senior Gold Director) wa kampuni hiyo ya Oriflame alisema vipodozi vya Ecollagen vimetengezwa kwa teknolojia ya kisasa zaidi isiyo madhara kwa watumiaji wa jinsia zote na hupunguza “uzee” katika ngozi kwa asilimia 49.

“Bidhaa zetu zimegawanyika katika makundi manne ya manukato ya kike na kiume,ya kulinda ngozi,(skin care),bidhaa za urembo wa rangi na kabla ya mteja kutumia hupewa kwanza ushauri wa kitaaalamu kwa kulingana na muonekano na afya ya ngozi yake”alisema.

Kampuni ya Oriflame ni ilianzishwa nchini Sweden miaka 50 iliyopita na ni kati ya makampuni makubwa yanayoongoza kwa utengenezaji na biashara ya vipodozi duniani ikisambaza biadhaa zake zake katika nchi zaidi ya 65 duniani

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...