Waganga wafawidhi ,bodi ya afya ,kamati za usimamizi wa vituo vya afya na zahanati pamoja na kamati za ulinzi wa mtoto kwa pamoja wametakiwa kuimarisha afya za mama mjamzito na mtoto na kufanikisha vifo havitokei.

Mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Dakaro(Daqqaro) ameyasema hayo mapema wakati akizindua kampeni ya JIONGEZE TUWAVUSHE SALAMA ngazi ya wilaya yenye lengo la kupunguza na kuondoa vifo vya mama na mtoto. 

Daqqaro(DAKARO) amesema kuwa miongoni mwa visababishi vya vifo kwa kina mama wajawazito ni uzembe unaofanywa na jamii husika,kutokufanya mazoezi pamoja na uzembe unao fanywa na baadhi ya watalamu wa afya ambapo amewataka watalaamu hao kuchunguza sababu ya ongezeko la kujifungua kwa opalesheni kwa kina mama .

Kwa upande wake kiongozi wa kimila mzee Tobikol amesema kuwa pamoja na serikali kuweka mipango mikakati ya kudhibiti vifo vya mama mjamzito bado baadhi ya vituo vya afya vina upungufu wa madakitali huku vingine vikiwa havifanyi kazi siku za wikiendi jambo ambalo huchochea ongezeko la vifo hivyo.

Naye Mganga Mkuu wa mkoa wa Arusha Wedsoni Sichalwe amesema kuwa chanzo cha vifo hivyo ni pamoja na Kifafa cha mimba,upungufu wa Damu kutokana na kupoteza Damu nyingi wakati wa kujifungua na baada ya kujifungua watoto kuzaliwa njiti na kushindwa kupumua.

Hata hivyo kampeni hii ambayo imezinduliwa Kiwilaya ni muendelezo ambapo Kimkoa ili zinduliwa tarehe 6 mwezi wa 4 mwaka huu na kitaifa ili zinduliwa tarehe 6 mwezi wa 11 mwaka 2018 kwa lengo la kuondoa vifo hivyo.
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqqaro akizindua kampeni ya JIONGEZE TUWAVUSHE SALAMA Kiwilaya uzinduzi uliofanyika katika ukumbi wa Goldenrose Jijini Arusha
Mganga mkuu wa Mkoa wa Arusha Dkt.Wedsoni Sichalwe akieleza vyanzo vya vifo kwa akina mama wajawazito.
Kiongozi wa kimila kutoka jamii ya wamaasai Njiani Arusha Mzee Tobikol akieleza baadhi ya changamoto zilizopo katika vituo vya afya mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Arusha mjini Gabriel Daqqaro katika uzinduzi wa kampeni hiyo.
Mganga mkuu wa jiji la Arusha Dkt.Simon Chacha aeleza sababu zinazopelekea mama wajawazito pamoja na watoto waganga kupoteza maisha ikionekana ni ucheleweshwaji wa mama mjamzito ngazi ya jamii kutokana na Mila na desturi katika kijamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...