Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amepongeza utendaji wa Bodi ya PSPTB na kueleza umuhimu wa kuundwa kwa Bodi hiyo ni pamoja na kusaidia wadau wapate bidhaa kwa wakati na kulingana na thamani ya pesa zao.
Aliongea hayo wakati alipotembelea banda la PSPTB na kuelezwa majukumu ya Bodi hiyo na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa PSPTB Godfred Mbanyi na hayimaye kukabidhiwa jarida lenye kuonesha kazi mbalimbali zilizofanya na PSPTB na muundo mzima wa Bodi ya wakurugenzi na menejimenti ya PSPTB.
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa akisoma moja ya jarida kwenye banda la bodi ya
ununuzi na ugavi(PSPTB) kuhusu jinsi bodi hiyo inavyofanya kazi wakati
wa ufunguzi wa wa Maonesho ya Vyuo vikuu yanayofanyika katika viwanja
vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kulia ni Kaimu
Mkurugenzi wa bodi ya ununuzi na ugavi(PSPTB) Godfred Mbanyi
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa
bodi ya ununuzi na ugavi(PSPTB) Godfred Mbanyi(katikati) kuhusu mfumo wa
usajili na jinsi bodi hiyo inavyofanya kazi wakati wa ufunguzi wa wa
Maonesho ya Vyuo vikuu yanayofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja
jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...