Na, Editha Edward-Tabora
Waziri wa nchi Tawala Za Mikoa na Serikali Za Mitaa TAMISEMI, Suleiman Jafo amefanya uzinduzi wa kitaifa wa shule shikizi nchini, Akizindua shule hizo kitaifa katika wilaya za Nzega na Igunga mkoani Tabora ambazo zimejengwa kwa ufadhili wa shirika la maendeleo la kimataifa DFID kupitia program ya EQUIPT
Waziri Jafo amesema ameridhishwa na utekelezaji wa miradi amepongeza mkoa wa Tabora kuwa miongoni mwa mikoa iliyofanya vizuri katika usimamizi wa miradi inayotekelezwa katika mikoa tisa hapa nchini na kueleza namna Serikali ilivyoridhishwa na matumizi ya fedha kiasi cha Shilingi bilioni Mia sita za program ya maboresho ya elimu nchini EQUIPT
Awali waziri Jafo pia alitembelea miradi mbalimbali ikiwemo mradi wa ufugaji mbuzi katika shule ya Msingi Isimba na mradi wa ufugaji samaki katika shule ya Msingi Simbo ambayo inafadhiliwa na DFID
Nae Mkuu wa mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri amesema upatikanaji wa Shule hizi utasaidia kuongeza Ufahulu kwa wanafunzi kwa kuwaondolea adha ya kutembea umbali mrefu kwenda shuleni huku mwakilishi wa shirika la DFID Elizabeth Arthy akibainisha kuwa shirika hilo limetenga kiasi cha Shilingi bilioni Mia sita katika utekelezaji wa miradi hiyo.
Pichani ni Waziri wa nchi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Suleiman Jafo, Akizungumza katika uzinduzi wa kitaifa wa shule Shikizi mkoani Tabora.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...