Picha ya Pamoja Mkuu wa Mkoa Kagera, Brig. Jen. Marco Gaguti pamoja na Wakuu wa Wilaya, wawakilishi wa Wakuu wa Wilaya, watumishi wa Afya, watendaji kutoka Wizarani, Mara baada ya uzinduzi wa kampeni ya Zero maralia inawezekaana
Pichani ni Katibu Tawala wa Mkoa Profesa Kamuzora, akitoa Maelezo machache kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Mkoa kuzindua rasmi kampeni ya zero maralia inaanza na Mimi, katika ukumbi wa E.L.C.T Bukoba.
Pichani Mwakilishi kutoka Wizara ya Afya maendeleo ya jamii, wazee jinsia na watoto Bi. Linda Makara akitoa shukrani zake kwa niaba ya Wizara, kwa Uongozi wa Mkoa juu ya utekelezaji wa masuala ya Afya Mkoani Kagera, katika Kikao cha Uzinduzi wa kampeni ya Zero maralia inaanza na Mimi.
Pichani Mwakilishi kutoka TAMISEMI Bwn. Kalidushi Charles nae akitoa shukrani zake kwa niaba ya Wizara jinsi Mkoa ulivyotekeleza na kusimamia masuala ya Afya ikiwemo ujenzi wa zahanati na Hospitali tatu za Wilaya.
Sehemu ya baadhi ya Viongozi wakiendelea kufuatilia Kikao maalumu cha uzinduzi wa Kampeni ya Zero maralia inaanza Mimi, katika ukumbi wa E.L.C.T Bukoba
Anaandika Abdullatif Yunus wa MichuziTV - Kagera.
Mkuu wa Mkoa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti amezindua rasmi Kampeni ya Kutokomeza maralia Mkoani Kagera itayoambatana na Ugawaji wa vyandarua kwa wanafunzi Shuleni inayobeba ujumbe wa "Zero maralia inaanza na Mimi"
Mapema Mhe. Gaguti akitoa salaam zake za ufunguzi amesema kitakwimu Mkoa wa Kagera, maambukizi ya ugonjwa wa Maralia kitakwimu ni asilimia 15.4 % ukilinganisha na asilimia 7% ya Maambukizi ya Maralia kitaifa, hivyo nakuongeza kuwa kama Mkoa juhudi kubwa imefanyika na inaendelea kufanyika kwani mwaka 2016 ambapo maambukizi yalikuwa asilimia 41% hivuyo kuwataka wasimamizi kuhakikisha maambukizi ya Maralia yanazidi kushuka zaidi.
Kampeni hiyo ambayo inaratibiwa na Ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa Kagera pamoja na Shirika la PSI chini ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee jinsia na watoto, na Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa inaaanza mara moja kwa kusambaza vyandarua shuleni, huku tahadhali ikitolewa juu ya matumizi ya vyandarua hivyo, na kwa yeyote ambaye atajaribu kukwamisha kampeni hiyo atakumbana na mkono wa sheria.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...