Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola, akikagua ujenzi wa darasa wa Shule ya Msingi Kamulebya, Kijiji cha Buzimbwe, Kata ya Butimba, Jimbo la Mwibara, Wilayani Bunda Mkoa wa Mara, wakati Mbunge huyo alipofanya ziara katika kijiji hicho kusikiliza kero za wapigakura wake pamoja na kuwataka wananchi wachape kazi. Waziri Lugola pia alitembelea miradi mbalimbali ya maendeleo, ikiwemo ujenzi wa madarasa ya shule na Zanahati. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Mkazi wa Kijiji cha Kamulebya, Kata ya Butimba, Jimbo la
Mwibara, Wilayani Bunda Mkoa wa Mara, Wambura Chacha Wambura, akimuuliza swali Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola (kulia), wakati Mbunge huyo alipofanya ziara katika kijiji hicho kusikiliza kero za wapigakura wake pamoja na kuwahamasisha kufanya kazi. Lugola aliwapa nafasi wananchi kutoa kero zao ndani ya Jimbo lake. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mwibara, Wilayani Bunda Mkoa wa Mara, Wambura Chacha Wambura, akimuuliza swali Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola (kulia), wakati Mbunge huyo alipofanya ziara katika kijiji hicho kusikiliza kero za wapigakura wake pamoja na kuwahamasisha kufanya kazi. Lugola aliwapa nafasi wananchi kutoa kero zao ndani ya Jimbo lake. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa
Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola (kushoto), akimsalimia Diwani wa
Kata ya Butimba, Jimbo la Mwibara, Wilayani Bunda Mkoa wa
Mara, Abyudi Mugesi, wakati alipokuwa anawasili Kijiji cha
Buzimbwe kwa ajili ya kufanya Mkutano wa hadhara na wananchi
wa Kijiji hicho. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Felix Mwagara, Mwibara (MOHA)
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amewataka wakazi wa Jimbo la Mwibara, Wilayani Bunda Mkoa wa Mara, kuilinda amani iliyopo nchini ili waweze kuendelea kufanya shughuli zao za kilimo wakiwa na amani.
Lugola ameyasema hayo leo, katika Kata ya Butimba, jimboni kwake, alipokuwa anazungumza na wananchi wa Kijiji cha Mwiseni, mara baada ya kushiriki shughuli za mazishi ya mtoto wa dada yake katika Kijiji hicho, aliyefariki hivi wiki hii mkoani Mwanza.
Lugola alisema Tanzania ina amani kwasababu inautamaduni wa kuwa na amani, hivyo asitokee mtu akaharibu utamaduni huo ambao nchi inaendelea kuhudumisha.
“Ndugu zangu wana Mwiseni, Wana Mwibara, amani tulionalo ndiyo inatuwezesha leo tunalima vizuri, tunavua samaki, leo tunakula vizuri, leo tunafanya shughuli mbalimbali za maendeleo, hivyo tuendelee kuitunza amani hii,” alisema Lugola.
Aliongeza kuwa, Wizara yake kupitia Jeshi la Polisi ipo imara, Serikali ya Rais Dkt. John Magufuli ipo imara na inaendelea kuwalinda Watanzania mahali popote walipo nchini, na hakuna mtu atakaye ivunja amani hiyo.
Aidha, Lugola aliwataka wananchi hao kuhifadhi vyakula vizuri ili kuepusha janga la njaa kwa hapo baadaye na kusababisha wananchi kuja kuteseka kwa ukosefu wa vyakula na kusababisha mateso katika familia.
“Tutunzeni vyakula vyetu, msitumie hovyo, kuweni makini na matumizi ya vyakula, sitaki nije kuona mnateseka na njaa, hakikisheni mnatunza vyakula kwa ajili ya matumizi ya baadaye, ogopeni njaa kama ukoma,” alisema Lugola.
Lugola ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo hilo, alifanya ukaguzi wa miradi ya maendeleo akikagua madarasa ya shule ya msingi pamoja na zahanati.
“Nataka hili darasa likamilike kwa wakati, natoa mifuko ya saruji 100 ili kuikalimisha zahanati hii katika Kata hii, na pia nitaleta mabati ili maendeleo yazidi kuwafikia wananchi wa jimbo hili,” alisema Lugola.
Waziri Lugola ameanza ziara yake leo, ambapo anatarajia kufanya ziara hiyo katika vijiji vya Kata zote jimboni humo.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...