Mamlaka ya Maendeleo ya biashara Tanzania (TANTRADE) imewataka wakulima na wafanyabiashara nchini kushirikiana nao kwa ukaribu ili kuweza kutatua changamoto mbali mbali ambazo wanakutana nazo katika shughuli zao.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya biashara Tanzania (TANTRADE), Edwin Rutageruka ameyasema hao leo, Julai 4, wakati wa ufunguzi wa Mikutano ya biashara Sekta ya Matunda na Mbogamboga katika maonesho 43 ya biashara yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na wadau mbalimbali, Rutegeruka amesema pamoja na mikakati ya Mamlaka pia kwa kishirikiana na wadau wengine ya kuendeleza bidhaa za Tanzania, yawapasa kutoa ushirikiano wa kutosha ili kutambulisha uwezo wa ubora wa kampuni katika kufanya biashara ili kutambulisha uwezo na ubora wa kampuni katika kufanya biashara ili waunganishe na fursa ambazo wanazipata.
Pia, Rutageruka amesema takwimu zinaonyesha kuwa thamani ya mauzo ya bidhaa za viwandani imeongezeka na kufikia dola za Marekani milioni 794.6 mwaka 2018 kutoka dola milioni 693.7 mwaka 2017, sawa na ongezeko la asilimia 14.5
Amesema, takwimu zinaonyesha kuwa Tanzania ina takribani viwanda 49,243 ambavyo kati yake, 393 ni viwanda vikubwa ambavyo vilivyopata usajili mwaka 2016/2017. Viwanda hivyo vilivyosajiliwa miongoni wao ni viwanda vinavyozalisha bidhaa mbalimbali ikiwemo usindikaji wa matunda na mbogamboga lakini bado vinakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa malighafi kutokana na upungufu wa uzalishaji wa ubora wa matunda,mboga, maua na viungo.
Aidha, Rutageruka amesema, nchi iko katika mwaka wa tatu wa utekelezaji wa mpango wa pili wa maendeleo wa miaka mitano wa mwaka 2016/2017-2020/2021, unaolenga kujenga uchumi wa viwanda ili kuchochea mageuzi ya kiuchumi na maendeleo ya Watanzania.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...