Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
Wizara ya Mifugo na Uvuvi imengara katika Maonesho ya 43 ya Biashara Kimataifa kwa kuwa mshindi wa Tatu katika kundi la Wziara zinazoshiriki maonesho hayo.
Akizungumza na Michuzi Blog Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Rehema Mbulalina amesema kuwa ushindi huo umetokana na wizara kujipanga na kuahidi kuboresha zaidi na kuwa mashindi wa kwanza maonesho yajayo ya 2020.
Amesema kuwa wananchi watembelee banda la Wizara hiyo katika kupata elimu mbalimbali ikiwemo sekta ya Mifugo na Uvuvi. Rehema amesema kuna mabadiliko mbalimbali yameganyika katika sekta hizo katika kwenda na mahitaji ya wananchi. Aidha amesema kuwa katika sekta ya Mifugo na Uvuvi zinakwenda sambamba katika uchumi wa Viwanda ambapo ni fursa ya wadau kuchangamkia kuwekeza sekta hiyo.
Kwa upande Wakala ya Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA) limewataka wananchi na hasa wavuvi kujitokeza kwa wingi Wizarani kuchukuwa fomu za kujiunga na kozi fupi za ufugaji wa samaki na ulinzi wa Mazingira. Wamesema kuwa kuna haja ya wananchi kujua namna ya kufuga samaki ili kuweza kupata tija katika mradi wake kuliko kufanya shughuli hiyo kimazoea.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Idara ya Ufugaji viumbe kwenye Maji Emmanuel Magesa amesema kuwa Wakala wanatoa kozi mbalimbali zikiwemo fupi na ndefu hivyo wananchi na hususani wavuvi wajitokeza kwa wingi ili kuchangamkia fursa hiyo.
"Jukumu kubwa la FETA ni kutoa elimu katika upande wa Uvuvi kwani waje wananchi katika Ofisi z Wizara na katika maonyesho ya sabasaba ili kupata fomu na kusoma kozi zinazohusika ufugaji" alisema. Amesema kuwa kuna kozi zinazohusika watu walioishia kidato cha nne ambao watasoma kwa mwaka mmoja na wale wakidato cha sita watasoma kwa miaka miwili na akifanya vizuri anapata fursa ya kwenda chuo kikuu.
Alisema moja ya kozi ni kama vile ufugaji wa samaki,kuogelea,kutengeneza nyavu,mitambo ya baharini,pamoja na usimamizi wa Mazingira hivyo wajitokeze kuchukuwa fomu na wajiunge na kozi hizo.
Pia alisema Wakala ya Elimu na Mafunzo ya Uvuvi FETA wanafanya tafiti mbalimbali za Uvuvi wa samaki na usimamizi wa rasilimali za bahari. Alisema lengo za tafiti hizo pia nikuongeza thamani katika.mazao ya bahari na kumekuwa na mwitikio mkubwa na wananchi wamejitokeza kwa wingi katika kufahamu ufugaji wa samaki ardhini .
"Kimsingi watu wamezoea kuona katika samaki wanapatikana baharini ,Mito,pamoja na maziwa lakini sasa mahitaji ni makubwa hivyo wananchi wanaingia ufugaji wa ardhini"alisema
Wananchi wakipata maelezo kuhusiana na Ufugaji wa Samaki katika eneo dogo wakati walipotembelea banda la Wakala ya Elimu ya Mafunzo ya Uvuvi (FETA) katika Maonesho ya 43 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Idara ya Ufugaji Viumbe Majini Wakala ya Elimu ya Mafunzo ya Uvuvi (FETA), Emmanuel Magesa akizungumza na muandishi wa habari katika Maonesho ya 43 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Ufugaji wa Samaki katika Maonesho ya Sabasaba.





Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...