Na Zainab Nyamka, Michuzi TV

SHAHIDI wa kesi inayowakabili viongozi wa Simba, ambaye ni Mchunguzi Mkuu kutoka TAKUKURU Frank Mkilanya, amedai kuelezwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya usajili wa Klabu ya Simba Zackaria Hanspoppe kuwa alitumia fedha zake binafsi dola 32,316.64 kulipa malipo ya awali wakati wa ununuzi wa nyasi bandia za klabu hiyo.

Ameyaeleza hayo leo Agosti 20,mwaka 2019, wakati anatoa ushahidi wake katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba.Ushahidi huo ni katika kesi inayowakabili waliokuwa viongozi wa klabu hiyo.

Akiongozwa na Wakili wa Serikali kutoka Takukuru Leonard Swai, Shahidi huyo alipewa maelezo na Hanspope kuwa katika ununuzi wa nyasi hizo yeye binafsi ndiye alianzisha mchakato wa ununuzi wa nyasi hizo na kufanya mawasiliano kati ya mnunuzi na muuzaji.

"Nilihusika kuandika maelezo ya Hanspoppe, kesi ilianza kufunguliwa kabla ya kuandika maelezo yake kwani mshitakiwa alikuwa hajapatikana, baada ya kupatikana ndio maelezo yake yakachukuliwa na hayo ndiyo alinieleza"alidai Mkilanya

Alidai katika maelezo hayo, mshitakiwa huyo pia alimueleza walinunua nyasi hizo kutoka kwa wakala aliyemtaja kwa jina la Hamis kutoka nchini China ambaye alinunua nyasi hizo kutoka Kampuni ya Ninah Trading Company.

Alidai, hundi ya manunuzi ya nyasi inaonesha zilinunuliwa kwa dola 109,499 ambapo Hanspoppe baada ya kupata hundi hiyo alifanya malipo ya awali ya dola 32,316.64 kwa fedha zake binafsi.

Mkilanya alidai,mshitakiwa huyo alimueleza kuwa hundi hiyo baadaye alimkabidhi aliyekuwa rais wa klabu hiyo Evance Aveva na kuna siku wakala (Hamisi) alikuja nchini na kumpa fedha taslimu dola 15,000.

Aliendelea kwa kueleza Hanspoppe alimueleza wakala huyo kwasasa aliyefanikisha ununuaji wa nyasi hizo amefariki.

Kesi hiyo itaendelea kusikilizwa Agosti 22 mwaka huu.Mshitakiwa mwingine katika kesi hiyo ni aliyekuwa Makamu wa rai wa klabu hiyo Godfrey Nyange maarufu Kaburu.

Washitakiwa hao wanakabiliwa na mashitaka 10 ikiwemo kula njama, kughushi, kuwasilisha nyaraka za kughushi, kutoa maelezo ya uongo na utakatishaji wa fedha.

Katika mashitaka la kughushi linawakabili washitakiwa wote, anadaiwa katika tarehe hizo hizo kwa pamoja walighushi hati ya malipo ya kibiashara ya Mei 28, 2016 wakionyesha kwamba nyasi bandia zilizonunuliwa na Simba zinathamani ya dola 40,577 sawa na zaidi ya Sh milioni 90 huku wakijua kwamba sio kweli.

Pia katika mashitaka mengine inadaiwa Aveva, Nyange na Hans Poppe kati ya Machi 10 na Septemba 30, 2016 waliwasilisha nyaraka za uongo kuonyesha Simba imenunua nyasi bandia zenye thamani ya Dola za Kimarekani 40,577.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...