Na Karama Kenyunko, Michuzi Tv.
MFANYABIASHARAKhamis Luwonga maarufu kwa jina la Meshack (38), anayedaiwa kumuua mkewe kwa kumchoma moto kwa kutumia magunia mawili ya mkaa, Naomi Marijani ameiomba Mahakama ya Hakimu Kisutu kuwa apatiwe Line zake mbili za simu zenye zaidi ya Sh. Milioni 5 kwa ajili ya matumizi ya nyumbani kwake pamoja na kumlipia ada mwanae.

Said ambaye ametinga mahakamani hapo akiwa na pingu miguuni kufuatia hivi karibuni kutoa vitisho mahakamani hapo kwa waandishi wa habari kwamba atawafanya kitu mbaya ametoa maombi hayo leo Agosti 27,2019 mbele ya Hakimu Mkazi, Salum Ally.

Mshtakiwa Said ametoa maombi hayo baada ya Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon kudai kuwa, Kesi hiyo leo imeitishwa kwa ajili ya kutajwa, upelelezi bado haujakamilika,

Baada ya kueleza hayo, Said alinyoosha mkono na kumueleza Hakimu kwamba ana mambo mawili muhimu ikiwemo nakala yake ya Hati ya Mashitaka na Line zake za simu zilizopo kituo cha kati cha Polisi (Central) na kuomba apatiwe line hizo zenye zaidi ya Sh.Mil 5 ili ziweze kutumika kwa matumizi madogo madogo pamoja na kumlipia ada ya mwanae.

"Sitaki simu ila naomba nipatiwe line ambazo nimpatie ndugu yangu atoe hizo hela kwa ajili ya matumizi, ikiwezekana zitolewe hata Polisi wakiwepo,"amedai.

Baada ya kueleza hayo, Wakili Wankyo ameeleza kuwa simu hizo ni sehemu ya upelelezi hivyo kwa sasa itakuwa ngumu kumpatia kwa sababu hawawezi kuamini moja kwa moja kama kweli anahitaji kutoa hizo hela.

Pia ameeleza kuwa kesi hiyo ni ya mauaji na maombi hayo alipaswa kuyawasilisha katika Mahakama husika yenye mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo ambayo ni Mahakamani Kuu na pia kama anahitaji fedha hizo basi atumie njia ya kumuandikia barua Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP).

Kufuatia maelezo hayo, Hakimu Ally alimshauri Said kutumia mbinu ya kuandika barua na kesi hiyo imeahirishwa hadi Septemba 10, 2019.

Katika kesi hiyo, mshtakiwa anatuhumiwa kwa kosa moja la mauaji Kinyume cha Sheria ya kanuni ya adhabu namba 196 sura 16 kama kilochofanyiwa marejeo mwaka 2002

Katika kesi hiyo ya muaji namba 4 ya mwaka 2019, mshtakiwa Luwonga ambaye ni Mkazi wa Kigamboni, Dar es Salaam anadaiwa Mei 15, 2019 akiwa Gezaulole eneo la Kigamboni alimuua Naomi Marijani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...