Charles James, Michuzi TV

TIMU ya Soka ya Dodoma Jiji Fc,inatarajia kushuka dimbani kesho kucheza  mchezo wa kirafiki dhidi ya Lipuli ya Mkoani Iringa,mtanange unaotarajiwa kufanyika katika uwanja wa Jamhuri Jijini hapa.

Huu unakuwa mchezo wa pili wa kirafiki ambapo hivi karibuni timu hiyo ilicheza na Mbeya City ya Mkoani Mbeya na timu hizo kutoka sare ya kutofungana.

Dodoma Jiji Fc inatarajiwa kukata utepe wa Ligi daraja la kwanza kwa kucheza na Reha Fc mchezo unaotarajiwa kufanyika Septemba 14 mwaka huu katika uwanja wa Jamhuri Jijini hapa.

Akizungumza Jijini hapa, Kocha Mkuu wa timu hiyo, Mbwana Makata alisema mchezo huo ni maandalizi kwa ajili kukipima kikosi chake.

" Tumepanga kucheza Michezo nane ya kujipima nguvu kabla hatujaanza Ligi, tunaamini kupitia Michezo hii tutaona mapungufu na kuyafanyia kazi, lengo letu ni kuhakikisha tunafanya vema na kuipandisha timu Ligi Kuu.

" Hamasa ni kubwa sana kwa wachezaji, tuwaombe mashabiki wetu kujitokeza kwa wingi, wao ni sehemu yetu na wingi wao ndio chachu ya sisi kufanya vizuri,"alisema.

Makata ambaye amewahi kuzifundisha timu kadhaa za Ligi daraja la kwanza na Ligi Kuu,alisema wamepanga kucheza Michezo nane ya kirafiki kabla ya kuanza kwa Ligi daraja la kwanza.
Kocha wa Dodoma FC, Mbwana Makata Akizungumza na wachezaji wake katika mazoezi ya Timu hiyo yanayofanyika katika uwanja wa Jamhuri

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...