Balozi
wa Uturuki nchini, Ali Davutoglu (katikati) na Mkurugenzi wa shirka la
ndege la Uturuki nchini, Ahmet Sahin (Kushoto), wakimkabidhi
Mkurugenzi wa Vodacom Business Unit Arjun Dhillon, mfano wa ndege
kuashiria uzinduzi rasmi wa huduma ya malipo kwa M-Pesa ambayo wateja
wao watapata punguzo la bei kwa asilimia 15 pindi wanaponunua tiketi ya
ndege kutoka shirika hilo, kuanzia tarehe 1 Agosti hadi Disemba Mosi
mwaka huu. Ofa hiyo ilitangazwa katika hafla fupi iliyofanyika ofisi za
Ubalozi wa Uturuki jijini Dar es Salaam jana.
Balozi
wa Uturuki nchini, Ali Davutoglu (katikati) na Mkurugenzi wa M-commerce
wa Vodacom Tanzania Epimack Mbeteni (wa kwanza kulia) na Mkurugenzi wa
Vodacom Business Unit, Arjun Dhillon (wa pili kulia), wakimsikiliza
Mkurugenzi wa shirka la ndege la Uturuki nchini, Ahmet Sahin, ( wapili
kushoto) akielezea punguzo la bei kwa asilimia 15 kwa wateja pindi
wanaponunua tiketi ya kusafiria kutoka shirika la ndege la Uturuki
(Turkish airline) kupitia huduma ya M-Pesa kuanzia tarehe 1 Agosti mpaka
Disemba Mosi mwaka huu. Ofa hiyo ilitangazwa katika hafla fupi
iliyofanyika ofisi za Ubalozi wa Uturuki jijini Dar es Salaam jana.
Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na shirika la ndege la Uturuki (Turkish Airlines), wametangaza ofa ya punguzo la bei kwa asilimia 15 kwa kila mteja atakaye nunua tiketi kutoka shirika hilo kupitia huduma ya M-Pesa, Ofa hii ni kuanzia tarehe 1 mwezi wa nane mpaka tarehe 1 Disemba mwaka huu. Ofa hii ilitangazwa katika hafla fupi iliyofanyika ofisi za Ubalozi wa nchi hiyo jijini Dar es Salaam, na kuhudhuriwa na Mheshimiwa Balozi wa Uturuki nchini, Ali Davutoglu na Mkurugenzi wa M-Pesa Bwana Epimack Mbeteni.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Vodacom Business Unit, Arjun Dhillon, M-Pesa Vodacom Tanzania, Epimack Mbeteni , alisema ubia huo umelenga kuchochea malipo ya kifedha kupitia njia za kidijitali kwa kuwawezesha wateja wao kufanya malipo kwa urahisi wanaponunua tiketi za ndege kutoka shirika la ndege la Uturuki (Turkish Airline) na kuelekea sehemu yeyote duniani wakianzia safari zao Tanzania.
“Tuna wajibu wa kutengeneza bidhaa na huduma za kifedha ambazo zinakidhi mahitaji ya watu binafsi na biashara, kama shirika la ndege la Ututurki. Ulipaji kupitia M-Pesa ni njia rahisi zaidi ya kufanya malipo; wateja wetu watafurahia faida za kulipia tiketi zao mda wowote na wakati wowote kupitia M-Pesa ukizingatia wanazawadiwa pindi wanapofanya malipo”, alisema Arjun
Akizungumza juu ya ofa hiyo Mkurugenzi wa shirka la ndege la Uturuki nchini, Ahmet Sahin, aliwapongeza Vodacom kwa kutumia teknolojia yao kuchochea huduma za kidijitali nchini. Sahin aliongeza kuwa huduma hii ni yakipekee kwa wafanyabiashara nchini Tanzania kulipia usafiri wa ndege kwenda Uturuki au maeneo 312 ambayo ndege zake zinafika, pamoja na kufaidika kibiashara na kujionea vitu ambavyo nchi zingine zinafanya (exposure).
“Wateja ambao watanunua tiketi za shirika la ndege la Uturuki kuanzia tarehe moja mwezi wa nane mpaka Disemba mosi watapata, sio tu pungufu ya bei kwa asilimia 15% kwa safari zote zinazoanzia Dar es Salaam, Zanzibar na Kilimanjaro, bali pia watafurahia huduma zinazotolewa kwa masaa 24 kutoka kwa watoa huduma wetu nchini kote. Napenda kuwahimiza wafanyabiashara, watalii na wateja wetu wote kutumia fursa hii,” alisistiza Sahin.
Shirika la ndege la Uturuki linaruka kwenda maeneo 312 katika nchi 126 duniani na ofa hii inahusu safari zote zinazoanzia nchini Tanzania kuelekea maeneo hayo.
Vodacom Tanzania Plc inaendeleza nia yake ya kuhakikisha kwamba kila Mtanzania anafaidikia na huduma bunifu zitokanazo na mtandao wa simu, vile vile kufungua fursa za kidijitali kwa Watanzania hasa wakati huu tukielekea kuinua uchumi wa nchi kuwa wa kati ifikapo mwaka 2025.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...